Wakuu, ijumaa nilipiga kwata kwenda Kidugalo, ni km 97 toka Ubungo mpaka huko, barabara ni nzuri sana kwa viwango vya Kitanzania. Nchi huko ni kubwa sana ila population hakuna. Kuna swine wa porini hadi uwanjani kabisa, watu ni wavivu hadi una kasirika. Mahindi yanaota vizuri, lakini yote yamelimwa na wageni ambao ni walimu na mwinjilisti wa Kanisa. Ni taasisi moja tu iliyojikatia pande huko, tatizo la Kidugalo/Mtakayo ni maji, maji hakuna, ila ukichimba mabondeni waweza pata. Kidugalo hakuna wafugaji, hata mbuzi hakuna.
Nilipata fursa ya kuonana na mwenyekiti, alisema ukitaka pande basi unaomba kijijini kwa kulipia fee, kwa taasisi wanapewa bure kabisa eka 50. Taasisi za dini waliopo pale wameshaomba.Ili kufuga kule inabidi uchimbe kisima bila hivyo wanyama watastawi masika tu. Umeme unapitishwa kwenda Mango, kwa sasa uko Mzenga. Kama ni shamba la kulima mazao kwa kutegemea mvua, basi Kidugalo ndo kwenyewe. Hindi hindi na hogo hogo kweli kweli.Wavamizi wapo na wameshajikatia mipori. Hapa kwa wajanja, unaweza kupata eneo na ukafungua godown lako. Usafiri upo kuanzia Buguruni Dsm. Mchanga wa kujengea huko ni tatizo kwa sehemu kubwa.
Nikijaliwa nitawaletea habari za mipori ya Kidunda nikijaliwa kupata Muda.