Mh, hii ngumu kweli kwetu watanzania, ni nani tanzania anaweza kuandaa kitu kikapokewa na positive mazee?
Yaani inavunja moyo kweli
Tatizo kubwa kama msemaji mmoja alivyo tangulia kusema ni tatizo la wanansiasa wetu, Tanzania inaongozwa kisiasa zaidi ya kitaalamu au kitaluma.
Tanzania matatizo tuliyo nayo ni hapo wanasiasa uchwala watakapo dhibitiwa lazima tujiulize ni kwa nini wataalamu wetu wanakimbilia kwenye siasa(sihasa- wazungu wanasema politricks na si politics).
Hizi politricks na sihasa ndo zimetufikisha tulipo.
Kama mh. Komba anaweza kuimba uzuri wachama mlolile na akawa maarufu kuliko kina Dr.Shaba hujaona kuwa pana tatizo hapo?
wanasiasa haohao kama mh.Makamba akipata kijana au mtaalamu aliye bobea jambo la kwanza atapigwa vita mpaka akimbie nchi.
Kwani wataalamu wetu wengi walioko nje walikimbizwa na nini si ni huu ubabaishaji wa wanasiasa?
Hivyo basi tutaunda kongamano za kila aina kama hatutapata busara za kuchimgua mzizi wa matatizo hao tutakalia kupunguza matawi tu na mwisho hatutafika mahali popote.
Wanataaluma wetu sasa tusikimbilie jambo lolote kabla hatuja lekebisha mambo ya msingi ambayo yametufanya watanzania tuwe wageni katika nchi yetu.
Lazima nchi irudishwe kwa wananchi kwanza maana sasa hivi iko mikononi mwa wanasiasa kadha ambao wanafadhiliwa na watu kadha kwa manufaa yao na BIASHARA ZAO.