Kuunguruma kwa kongamano la Wanataaluma Dar: Moto wayaka!

Mh, hii ngumu kweli kwetu watanzania, ni nani tanzania anaweza kuandaa kitu kikapokewa na positive mazee?

Yaani inavunja moyo kweli

Tatizo kubwa kama msemaji mmoja alivyo tangulia kusema ni tatizo la wanansiasa wetu, Tanzania inaongozwa kisiasa zaidi ya kitaalamu au kitaluma.
Tanzania matatizo tuliyo nayo ni hapo wanasiasa uchwala watakapo dhibitiwa lazima tujiulize ni kwa nini wataalamu wetu wanakimbilia kwenye siasa(sihasa- wazungu wanasema politricks na si politics).
Hizi politricks na sihasa ndo zimetufikisha tulipo.
Kama mh. Komba anaweza kuimba uzuri wachama mlolile na akawa maarufu kuliko kina Dr.Shaba hujaona kuwa pana tatizo hapo?
wanasiasa haohao kama mh.Makamba akipata kijana au mtaalamu aliye bobea jambo la kwanza atapigwa vita mpaka akimbie nchi.
Kwani wataalamu wetu wengi walioko nje walikimbizwa na nini si ni huu ubabaishaji wa wanasiasa?
Hivyo basi tutaunda kongamano za kila aina kama hatutapata busara za kuchimgua mzizi wa matatizo hao tutakalia kupunguza matawi tu na mwisho hatutafika mahali popote.
Wanataaluma wetu sasa tusikimbilie jambo lolote kabla hatuja lekebisha mambo ya msingi ambayo yametufanya watanzania tuwe wageni katika nchi yetu.
Lazima nchi irudishwe kwa wananchi kwanza maana sasa hivi iko mikononi mwa wanasiasa kadha ambao wanafadhiliwa na watu kadha kwa manufaa yao na BIASHARA ZAO.
 

Ni kweli lakini nadhani wakati haujawa mwafaka kila jambo lina wakati wake na ninaamini mkuu mkjj hilo analijua wakati ukiwadia hatahitaji kuobwa kufanya hivyo mkuu.
 

Zakumi;Posting yangu uliyoijibu ambayo niliielekeza kwenye kuijibu post ya MKJJ,nilisema hivi....
Na katika pita pita yangu leo hapa jeo nimekutana na uchambuzi huu kutoka kwa profesa Issa Shivji kuhusiana na siasa za mwalimu...


Hitimisho langu liko pale pale,kama mentality ni ya kuomba omba bado na kumsubiria uncle sam etc hatutaweza kuprogress,ni mapambano ya kifikra,ni makovu yanayoambatana na jamii nyingi za kiafrika,ndiyo reality,tatizo kubwa la waafrika wengi ni wasahaulifu mapema,je kwenye sera yetu ya kuomba omba incentives za kutafuta ufumbuzi zitakuwa ni zipi hizo?
 

Mchungaji;

Niliyoyashuhudia nashindwa kuyaelezea. Kukiwa na namna nina DVD zilizorekord proceeds zote. It was very exciting.

Kunapokutana Wanataaluma wenye uchungu na nchi yao, kuna zaidi ya utakayodhania. Kama watu wametoka ughaibuni kuja kuhudhria Kongamano hili, huku wamejilipia nauli, malazi, na gharama za hoteli nk. kisha partcipation fees, mchana hawajali hata muda wa kula kwa kuwa wana issues muhimu za kujadili, muda wa kumaliza kikao umefika, wanataka waendelee hadi usiku na hapo hawalipwi per diem, hakika si kitu cha kawaida.

Na ni nani aliyesema Wazalendo Nchi hii waekwisha au hakuna uzalendo?

Napenda kukuhakikishia kuwa, yote yanayoweza kutekelezeka chini ya Mtandao wa wanataaluma yatafanyiwa kazi.

Taarifa zaidi, kong'oli hapa:
https://www.jamiiforums.com/habari-...luma-waishio-ndani-na-nje-ya-nchi-2009-a.html
 

Lakini hujajibu swali (maswali) langu....!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…