Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,181
- 1,579
Suala la kuuza au kutouza nafaka nje.
Yaani niseme kwamba; kulingana na kiwango kidogo cha chakula tulichonacho, sikubaliani na wale wanaotaka tuuze chakula nje. Ndugu zangu msifikiri jambo hili ni rahisi kama mnavyoliona, mkaanza kuilaumu serikali kwa zuio lililopo.
Mtu yeyote mwenye akili timamu; kwanza anajitoshereza mwenyewe, kisha kilichozidi ndicho hukiuza kwa mwenzake.
Utakuwa ni upunguani wa kifkra, kama taifa, tukiuza chakula kwa shilingi, kisha baada ya miezi michache tukatumia akiba ya madola kuagiza chakula hichohicho nje ya nchi.
Pili, ni kweli wakulima wetu wataumia kidogo, nasema kidogo kwa sababu hata wao chakula hiki kitawasaidia baadaye, maana wanauzaga mpaka akiba kwa tamaa ya bei ya angalau, ndiposa baadaye wanateseka sana kwa njaa.
Nasema bei ya angalau kwa sababu kwa kweli mnufaikaji mkubwa wa hili ni mlanguzi.
Tatu, Ukiangali kwa jicho la tatu; sehemu kubwa ya nchi yetu mavuno hayakwenda vizuri. Yaani watnzania wengi hawana chakula.
Utaona ni kipindi cha mavuno lakini bado maeneo mengi bei za chakula hazijarudi mahala pake.
Hivyo ilikuwa vema kama taifa tuamue kuwaumiza wengi au wachache. Sawasawa na dereva wa basi atakayeamua kumkwepa mtu mmoja akaangusha basi zima, au kumgonga huyo na kusalimisha 65.
Mwisho, kulinga na ukame mkubwa unaoendelea kuzikumba nchi nyingi za ukanda huu wa afrika mashariki na kati, siyo vema kutegemea manchi haya makubwa yauziwe chakula na wananchi wanaojilimia kienyeji tu.
Ni kwa nini usifanyike uwekezaji mkubwa kulingana na fursa iliyopo, utakaokidhi hitaji la soko lililopo?
Kwa sababu haiwezekani chakula cha nchi moja kikategemewa na ma…nchi kibao huko ni kutengeneza njaa kwa wahusika wenyewe!
Ungekuwa wewe ni mfanya maamuzi ungefanyaje?