Kuuza eneo ambalo bado halijapata certificate of offer


Haya Mwanasheria.
Nimechangia tu pale napodhani ni sahihi maana mnasema kila raia anapaswa kuifahamu cjui kuzfaham sheria za nchi yake na washirika.
 

Sasa nisaidie jibu atauza vipi ilihali hana hati wala doc za umiliki halali wa hiyo Ardhi!?
 
Wewe wacha kupotosha.. Hii kitu imekuwa repealed na sheria namba 17 ya 2008 S.5

Ndio maana hapo mwanzo nimesema mlikuwa mnaenda kinyume na matakwa ya Sheria.

Mkuu hizi Letter of Offer zinatumika na binafsi nina maeneo mawili Manispaa mbili tofauti na kote mfumo wa Letter of Offer unatumika ambapo unakuwa issued hii kisha mnasubiri ramani ya block husika ikitoka ndipo na processes za kupata hati ya ardhi unafuatia
 
Wewe wacha kupotosha.. Hii kitu imekuwa repealed na sheria namba 17 ya 2008 S.5

Ndio maana hapo mwanzo nimesema mlikuwa mnaenda kinyume na matakwa ya Sheria.

Naona umehamia kwa mtu mwingine...hyo sheria ya ardhi ya 2008 inaitwaje...cite jina la hyo Act tafadhali.
 
Wewe wacha kupotosha.. Hii kitu imekuwa repealed na sheria namba 17 ya 2008 S.5

Ndio maana hapo mwanzo nimesema mlikuwa mnaenda kinyume na matakwa ya Sheria.
Sorry kumbe napotosha, anyway mie nilipewa LETTER OF OFFER baada ya kukamilisha malipo , of curse ilikuwa 2007 na letter of offer niliitumia kwa kufuatilia hati yangu 2009 hivyo kwangu ni ngumu kujua kama kuna mabadiliko. Kwahiyo nikinunua kiwanja sasa hivi napewa nini maana Halmashauri / Manispaa / Jiji kazi yake kupima viwanja na kuuza ambapo ulikuwa ukimaliza unapewa letter of offer na Manispaa/jiji alafu baadae hati yako unaifuatilia kwa kamishina wa ardhi. (kwahiyo kwa sasa kuna nini mkuu kwa sababu kwenye masuala ya ardhi so mtaalamu wa ardhi ila nina practical experience ya utumiaji wa ardhi na document zake nadhani itakuwa vyema kama ukitutajia mbadala wa letter of offer na mahusiano ya hizi idara mbili mtoa hati ambae ni kamishina wa ardhi na muuza viwanja ambae ni manispaa, halmashauri za wilaya na majiji)

Ahsante Cathode Rays
 
Last edited by a moderator:
Sasa nisaidie jibu atauza vipi ilihali hana hati wala doc za umiliki halali wa hiyo Ardhi!?

I said from the very beginning kwamba " aende halimashaur husika kama atazuiliwa kuuza kwa sababu ya taratibu hzo mpya basi apate hyo offer kwa sababu tayar ina andaliwa then, baada ya kupata offer itachukua mda mfupi kupata GRO kama kweli atakua serious... Lakin ninachojua watu huwa wananunua offer afu yule anaye nunua kwa sababu ndo ataendelea kumiliki anatafuta RO "principles of equity" lakin siyo kumkatalia mtu asiuze ilihali kuna vgezo vnamuoneshwa ni mmiliki mtarajiwa wa eneo lile na alitoa hela za kulinunua...ukimkatalia where is fairness??.
 

Kwanza nakuunga mkono mkuu, Pia ukisoma maelezo ya huyo mleta uzi kidogo kuna utata kwa kuwa na yeye hayupo aware na mambo ya ardhi, kimsingi kama kiwanja amekilipia ile letter of offer alitakiwa awe nayo mkononi mara tu alipomaliza na mara nyingi ukishalipia unapeleka picha 4 kama sikosei alafu unasaini zile letter offer na unaambiwa uje baada ya siku kadhaa kuja kufuata letter of offer yako kwa kuwa inatakiwa ipite kwa maafisa kadhaa kitu ambacho kwa siku hiyo hiyo haiwezekani.

Kwa kumsaidia huyu kamanda naungana na wewe pia kuna mistake ndogo aliifanya ya kutokwenda kuichukua kwa wakati offer yake hivyo kama ana receipt zote za manunuzi anatakiwa aende kwenye Manispaa ya Kinondoni na receipt zake watampa letter of Offer ambayo hiyo ni mali yake wala haitakiwi kubaki kule manispaa kwa kuwa na wao wana copy zao tena tatu alafu akishapata ile offer baadae anatakiwa sasa afuatilie hati (kimsingi ukshapewa offer baada ya miezi 6 unatakiwa upewe hati ila kwa kuwa watumishi wa serikali mambo mengi inabidi ufuatilie tena hapo hapo Kinondoni kwa kuwa Manispaa huwa right of occupance kujua kama zimepelekwa kwa kamishina wa ardhi kama bado atakupa mwongozo mara nyingi mnaweza enda nae au akakupa ukaenda kwa mwanasheria ambae ana approve kama ni wewe na kukugongea mhuri kisha unamrudishia (zinakuwa mbili na duplicate yake) kisha yeye ataipeleka kwa kamishina wa ardhi (I guess kwa Dar zinapelekwa wizarani ila sehemu zingine kuna makamishina wa ardhi), kazi yako wewe ni kwenda kwa kamishina kuhakikisha kama hati yako imesajiriwa na kama imesajiriwa utasaini kwenye logbook na kuanza na kupewa tarehe ya kurudi tena (ambapo wale ambao hati zao tayari majina yao yanabandikwa ukutani na kama bado unaulizia mpaka watakupatia)

Mleta uzi atakuwa alipolipia tu na kupewa zile receipt hakufuatilia offer (kwahiyo pita ofisini Kinondoni na receipt zako watakupa offer

Pia served katika comment #5 ameeleza vizuri, kama huna hati lazima mwende wote Manispaa kuhakikisha kwamba kiwanja ni chako alafu taratibu za umilki kwa mwingine zinafanyika wakati kiwanja kimeuzwa (na ndio maana inashauriwa ukiwa na offer hata kama kiwanja kimepimwa na umekilipia bado unatakiwa uwe na hati ili utakapokiuza ni kwenda kwa mwanasheria tu yaani kama vle unapokuwa na kadi ya gari mnapouziana lakini ukiwa huna hati lazima mwende halmashauri then process iwe ndefu kama hiyo lakini biashara mnafanya tu bla shida)
Cathode Rays njoo utoe uzoefu maana inabidi sie tusiojua sheria tutoe uzoefu wetu alafu wazee wa sheria nao watoe maandiko yao
 
Last edited by a moderator:

CC Cathode Rays
 
Last edited by a moderator:
Kazi yako ni moja tu ambayo ni CC, mwaga nondo mkuu Asprin

Mkuu mimi ni layman kwenye haya mambo. Mi hutumia kijana kufuatilia haya mambo. Ngoja nikatafute experience kwake labda ntaweza kuja kumwaga nondo.

Ila unachokisema wewe ndio kama ambacho kinafanyika.

Ngoja ntarudi niangalie hiki nlichobahatisha Mabwepande hivi majuzi mambo yaliendaje.
 
Mkuu mimi ni layman kwenye haya mambo. Mi hutumia kijana kufuatilia haya mambo. Ngoja nikatafute experience kwake labda ntaweza kuja kumwaga nondo.

Sie ma-layman ndio wazuri kwa kuwa tunafuatilia hatua kwa hatua kwa kutoa na uzoefu na sio kusoma kwenye makaratasi, hata hivyo mleta uzi Kifaranga ana wasiwasi tu ukishapata ukishalipia kiwanja kila kitu kimejumlishwa mpaka gharama ya hati na mhuri na duplicate ya hiyo hati hivyo hakuna kodi yoyote zaidi ya kodi ya kiwanja ambayo haihusiani na hati, poa kiongozi
 
Last edited by a moderator:

Mkuu uko very right na sina cha kuongeza

That is how it works. Na moja ya makosa ya kizembe ni kutokuchukua Leter of Offer yako mapema na kwa wakati

Maafisa ardhi wetu walivyo mafisi usishangae mchezo ukachezwa.

Hii inatoa usalama hata kama bado hujawa na right of occupancy.

Anaesema hazitumiki kisheria napata ugumu kumuelewa maana Manispaa zote mbili nilizo na viwanja hizi Letter of Offer wanazitoa lakini zaidi ni miongoni mwa viambatanisho (backup) muhimu unapotaka ku-process vibali vya ujenzi. Najua wana wanasheria wa Manispaa zao na kama hazipo kisheria inakuwaje ziruhusiwe kutumika?

Hivyo mtoa mada tambua Letter of Offer ni za muhimu na fuatilia uipate na hakikisha unailipia kodi ya ardhi kila mwaka

Kwa nyongeza pia, kama ulivyosema mkuu Jodoki Kalimilo, mnaweza kuuziana kama una Letter of Offer bila shida yoyote.

Rafiki yangu mmoja kanunua kiwanja cha mtu kwa kutumia Letter of Offer.... of course ni ka process kidogo maana nilienda nae na alipewa maelekezo kuna kulipia lakini kama sikosei kuna amount fulani inabidi upeleke TRA ambayo ni asilimia kadhaa ya ile amount uliyolipia (I stand to be corrected maana sikumbuki vyote per ser).

Walienda Mahakamani kuprocess hiyo transfer na walipomaliza wakaenda Manispaa sasa kufacilitate mchakato wa kuhamisha umiliki kwenye files za Manispaa. Kisha huyu mmiliki mpya akatengezewa file lake na file la mmiliki wa zamani linabanwa nyuma ya file la mmiliki mpya
 
Last edited by a moderator:

Ahsante kwa elimu mkuu nadhani mfaranga angalau amepata pa kuanzia kwa 85% maana sie sio watu tunaojua yote, kazi njema mkuu
 
Last edited by a moderator:
Una mpango wa kukiuza bei gani? Cha msingi kama ni mauziano lazima yafuate taratibu za kisheria ambapo wewe utaonekana umeuza umiliki kwa mtu mwingine then huyo mmiliki mpaya ataendelea na mchakato wa kubadili jina na kufuatilia hati kwa jina lake
 

Ahsante kwa Elimu ya msingi kabisa katika masuala ya Sheria za Ardhi.

Ila nimegundua kitu hapa Jukwaa la Sheria, nyie wanasheria ni Wachoyo sana kutoa Msaada kwa wenzenu hapa Jf.

Mnapenda kujitokeza baada ya kuona mitifuano isiyo na Msingi.

Acheni hizo.

Cc Petro mselewa
 
Last edited by a moderator:

Mie nilijua na wewe ni mwanasheria kumbe na wewe ni kama sie, by the way mambo ya ardhi wengi tunahitaji kupewa ABC
 
Last edited by a moderator:

Kalimililo, soma case law hiyo utapata the real taste of the power of latter of offer:
SARJIT SINGH v SEBASTIAN CHRISTOM 1988 TLR 24 (HC) Court High Court of Tanzania - Dar Es Salaam
Judge Kyando J
Maelezo yako siyo sahihi, jitahidi usiandike mambo bila kujua fika unachokiandika. Utawapotosha watu. lakini umejitahidi kutuelimisha, asante
 
Naona umehamia kwa mtu mwingine...hyo sheria ya ardhi ya 2008 inaitwaje...cite jina la hyo Act tafadhali.

Mkuu muelewe uyo jamaa kwa kuwa letter of offer ilishacease na hazitolewi chini ya sheria ya ardhi . haipo tena vinginevo tuelezwe ni kifungu gani!!
 
Mkuu maamuzi ya mwaka88 yanaweza kufutwa na sheria yoyote ikiwa repealed. Mwaka 1999 ilitungwa sheria ya ardhi iliyo na nguvu zaidi ya mwaka88

...mfano kabla ya 99 land tribunal ruling zilikuwa unapoeallable. Baada ya sheria ya ardhi mpya iliondolewa. Ivo sheria zinaenda na wakati mkuu!!
 

Wewe mbishi soma kwanza hiyo case law then uje hapa. unabisha tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…