Mkuu uko very right na sina cha kuongeza
That is how it works. Na moja ya makosa ya kizembe ni kutokuchukua Leter of Offer yako mapema na kwa wakati
Maafisa ardhi wetu walivyo mafisi usishangae mchezo ukachezwa.
Hii inatoa usalama hata kama bado hujawa na right of occupancy.
Anaesema hazitumiki kisheria napata ugumu kumuelewa maana Manispaa zote mbili nilizo na viwanja hizi Letter of Offer wanazitoa lakini zaidi ni miongoni mwa viambatanisho (backup) muhimu unapotaka ku-process vibali vya ujenzi. Najua wana wanasheria wa Manispaa zao na kama hazipo kisheria inakuwaje ziruhusiwe kutumika?
Hivyo mtoa mada tambua Letter of Offer ni za muhimu na fuatilia uipate na hakikisha unailipia kodi ya ardhi kila mwaka
Kwa nyongeza pia, kama ulivyosema mkuu
Jodoki Kalimilo, mnaweza kuuziana kama una Letter of Offer bila shida yoyote.
Rafiki yangu mmoja kanunua kiwanja cha mtu kwa kutumia Letter of Offer.... of course ni ka process kidogo maana nilienda nae na alipewa maelekezo kuna kulipia lakini kama sikosei kuna amount fulani inabidi upeleke TRA ambayo ni asilimia kadhaa ya ile amount uliyolipia (I stand to be corrected maana sikumbuki vyote per ser).
Walienda Mahakamani kuprocess hiyo transfer na walipomaliza wakaenda Manispaa sasa kufacilitate mchakato wa kuhamisha umiliki kwenye files za Manispaa. Kisha huyu mmiliki mpya akatengezewa file lake na file la mmiliki wa zamani linabanwa nyuma ya file la mmiliki mpya