Kuuza wazo kwa makampuni ya simu

Kuuza wazo kwa makampuni ya simu

bnhai

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2009
Posts
2,832
Reaction score
2,390
Nina mawazo kadhaa kwa makampuni ya simu yenye kuongeza tija na mapato. Ninajiuliza hawa jamaa hununua mawazo na siku ya mwisho hakuna kuibiana? Ukitumia mwanasheria, huwa wanacomply kiasi gani. Nani mwenye uzoefu au njia. I believe the ideas are worth fortune.
 
Ni ngumu bro labda usajili patent copyrights kwanza
 
Linaweza kuwa replicated. Sidhani kwa patent. Basi ngoja nikaushe kama wanaweza kunitafuta fine. Nina hakika ni pesa nyingi saana beyond charging customers for photocopying.
 
Ilikuwa tarehe 24 December, 2007 nilipopigiwa simu na watu wa mtandao fulani wa simu (nisingependa kuutaja jina) nikitakiwa kwenda kuchukua zawadi ya X-mas kutokana na wao kuniona kama mmoja wa watu waliokuwa wakitumia sana huduma za mtandao wao kila siku. Nilipofika kwenye ofisi zao zilizokuwa ndani ya jengo la Barclays jirani na hotel ya Movenpick (siku hizi Dar es Salaam Serena Hotel) nilikutana na baadhi ya wateja wengine waliokuwa wamefika kuchukua zawadi zao ambazo nakumbuka ilikuwa ni saa ya ukutani yenye nembo yao, wine,pamoja na pipi kadhaa. Pamoja na kwamba hao wateja baada ya kuchukua zawadi zao walikuwa wakiombwa kuchukua kalamu na karatasi ili angalau watoe maoni yao kwa nia ya kuboresha huduma za mtandao huo lakini kiukweli wengi walikuwa wakiondoka bila kuandika maoni yoyote. Mimi niliamua kutumia zaidi ya dakika 45 nikiandika maoni yangu kwa umakini mkubwa. Nakumbuka niliandika maoni ya aina tatu. Baada ya miezi kama miwili nikaona kampuni hiyo iki introduce huduma ambayo ilikuwa ni kila kitu ya kile nilichokuwa nimeandika kwenye maoni yangu. Hiyo huduma pia ikaja kuigwa na kampuni nyingine shindani na hadi leo hii hiyo huduma ipo na naamini inawaingizia hela nzuri kampuni hiyo na hata ile kampuni shindani iliyoiga kwa mwenzie. Nilichojiuliza ni iweje kampuni kwa kutumia maoni niliyoyatoa isinitumie hata ka sms tu ka kuonyesha appreciation yao juu ya hayo maoni yangu waliyofanyia kazi?! Pengine nilikuwa mzembe kwa staili niliyotumia kutoa maoni yale. Lakini pia sipendi kujilaumu kwa uzembe huo.
 
Mh kwahiyo bongo km unajua kitu unatakiwa kutosema? Basi nitakaa kimya maana kwa hili, sipo tayari kuwaambia kuna cost implications kwa wateja.
 
Daaah pole mkuu mimi nina wazo zuri ambalo ni productive sana kwa hizi biashara za migahawa (restaurants) but kila ninapo jaribu kukaa na wamiliki wa migahawa kupiga nao soga na kuintroduce hiyo issue naona hakuna nzuri kwangu ya mimi kunufaika na wazo langu....Wengi wanaishia kukuambia tukuajiri then ni implement wazo langu kitu ambacho najua kitakua ni in short term benefits
 
Mkuu kwanini usifungue mgahawa ukatumia hiyo fursa... Kama vipi nidokeze PM teh...
 
Hizo ni kazi za watu wa product development unaweza kumtafuta muhusika wa kampuni husika ukaongea naye kiurafiki then anaweza akakutengenezea ulaji kama wazo lako litakuwa linalipa.
 
Back
Top Bottom