SI KWELI Kuvaa nguo nyekundu kunasababisha kupigwa na radi

SI KWELI Kuvaa nguo nyekundu kunasababisha kupigwa na radi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
1673611900113.png

Madai:
Yapo madai kutoka katika jamii mbalimbali yakihusisha rangi nyekundu na radi. Baadhi ya jamii zinaamini kwamba kuvaa mavazi yenye rangi nyekundu wakati wa mvua ni hatari kwa sababu yanaweza kusababisha ukapigwa na radi. Sambamba na hilo jamii nyingine zinaamini Mjusi kafiri na Kondoo wana uwezo wa kupambana na radi.
---
 
Tunachokijua
Radi ni mwangaza na miale ya mwanga mithili ya shoti za umeme inayotokea wakati wa ngurumo wa mvua ya radi. Neno radi linaweza kutaja pia sauti yenyewe na mwanga katikati ya mawingu unaweza kuitwa "umeme".

Asili yake ni volteji inayojijenga kati ya mawingu angani yenye chaji tofauti au pia kati ya mawingu na ardhi. Volteji hiyo ikiongezeka mno husababisha mkondo wa umeme hewani unaoonekana kama mwangaza mkali.

Mkondo unatoa pia joto kali na joto hilo husababisha kupanuka kwa hewa ghafla. Upanuzi huo unaleta sauti inayosikika kama ngurumo kama ni mbali, lakini inaweza kusikika pia sawa na mshtuko wa mlipuko kama ni karibu.
387px-Lightning_in_Arlington.jpg

Ni kweli kwamba kumekuwa na imani mbalimbali kwa jamii nyingi za Kiafrika Tanzania na Rwanda ikiwamo zinaitazama radi kijadi zaidi. Wapo wanaamini ni hatari kuvaa mavazi yenye rangi nyekundu wakati wa mvua kwa sababu mavazi hayo yanavutia radi kukufata. Hata hivyo, bado hakuna uthibitisho kamili unaobainisha chanzo cha jamii hizo kuamini hivyo. Kamazima Lwiza, Profesa wa fizikia ya anga New York Marekani akieleza hadithi za uongo na kweli, saba kati ya hizo anataja nguo nyekundu kuwa kuvutia radi kuwa ni hadithi ya uongo.

Zipo Imani nyingine kadhaa za kijamii kuhusu radi ambapo pia baadhi ya jamii za Afrika ya sasa na Ugiriki zamani zinaamini radi zinatengenezwa na watu au miungu inatumika kama silaha ya kijadi kuwashambulia wengine au kutoa adhabu.

Hoja zote hizi ni sehemu ya hoja nyingine nyingi za kijamii kuhusu radi. Lakini hazithibitiki kisayansi

Je, sayansi inasema nini kuhusu uhusiano wa nguo nyekundu na radi?

Wataalamu wa hali ya hewa wanaeleza kuwa kwa tafiti zilizopo mpaka sasa ulimwenguni hakuna uhusiano wowote kati ya radi na rangi yoyote Ile. Mathalani, Wilbert Kikwasi wa TMA anaeleza kuwa radi inatokana na tofauti ya nguvu za umeme kati ya mawingu na ardhi. Anaongeza kuwa hakuna uthibitisho wa kisayansi unaobainisha namna rangi nyekundu inavyoweza kuchochea au kuvutia radi.

Zaidi ya hayo, Wataalamu wa masuala ya hali ya hewa wanafafanua kuwa Radi hutokana na kuachiliwa kwa umeme tuli, tukio ambalo hutokea kutokana na tofauti ya nguvu za umeme kati ya mawingu na ardhi. Radi ni Umeme ambao husafiri kutoka juu hadi chini na kwa kawaida hugonga vitu virefu zaidi.

Mazingira ya kupigwa na radi yanategemea zaidi kama umekaa kwenye vitu virefu kama miti, milima, kwenye minara shamba au kwenye mimea mifupi ambayo umeizidi Kimo. Mara unapoona dalili za radi Inashauriwa kutotumia mwamvuli kujikinga na mvua zinazoambatana na radi kwani mwavuli utakufanya kuwa kitu kirefu kupita vingine kufanya wewe pamoja na mwavuli wako kuwa njia rahisi ya radi kuingia ardhini.

Kukaa ndani ya nyumba zilizowekwa vifaa vya kuzuia Radi inaweza kuusaidia kujikinga na dhidi ya radi pia Kukaa ndani ya gari kunaweza kukuzuia kupigwa na radi, lakini unashauriwa kufunga vioo na kutokushika kitu chochote chenye asili ya chuma ukiwa ndani ya gari, hapo utakua salama.

Pia wakati wa mvua zinazoambatana na radi ni vema kuepuka kunawa mikono kwa maji, kufua nguo, wala kuogelea au kuoga. Ni muhimu kuzima vifaa vya umeme kama vile TV, Radio, computer huku ukichomoa nyaya zilizounganishwa kwenye chanzo cha umeme, epuka kuchomoa waya wakati radi inapiga. Usitumie Simu za mezani zilizounganishwa na waya kutoka kwenye nguzo wakati wa mvua za radi kwani kuna uwezekano mkubwa ukapigwa na radi.​
radi-pc-data.jpg

Hakuna uhusiano wowote kati ya nguo za rangi nyekundu na kupigwa na radi, JamiiForums inasisitiza kuchukua hatua za kitaalamu za kujikinga na radi kama, kutokaa chini ya miti na majengo marefu wakati wa mvua.
View attachment 2334074

Madai:
Yapo madai kutoka katika jamii mbalimbali yakihusisha rangi nyekundu na radi. Baadhi ya jamii zinaamini kwamba kuvaa mavazi yenye rangi nyekundu wakati wa mvua ni hatari kwa sababu yanaweza kusababisha ukapigwa na radi. Sambamba na hilo jamii nyingine zinaamini Mjusi kafiri na Kondoo wana uwezo wa kupambana na radi.
---
Ngoja nikupe hii elimu kifupi sana itakufanya uachane na hizi imani, Iko hivi mawingu ya mvua kwa juu ni positive charged (+) na kwenye kitako/base yake yaani uanvyonyanyua kichwa chako juu kuyatazama mawingu juu ndo chini yake (base/kitako cha mawingo) so hii base ya chini ya mawingu ni negative charged in nature (-) sasa mkuu dunia yetu yaani ardhi ya dunia yetu ni positively charged in nature (+) kwahiyo tunajua alike charge (+) + (+) = repels each other/zinakwepana hivyo unlike charge (+) + (-) = attracts each other, kale ka mchezo ka kukwepesha sumaku zenye ncha zinazofanana na ambazo hazifanani zinavutana ndo katumie hapo kwenye mfano wa chaji za radi na ardhi..! Hivyo charge ya RADI huwa inavyutwa kuja duniani kwa sababu chaji ya radi ni hasi/- na ya dunia ni chaji ya chanya/..

............Sasa viumbe wenye madini mengi ya chumvi na chuma kama minyoo, hao mijusi, kuku na wengineo wenye madini rafiki ya kupitisha umeme ndo wako hatarini sana na vitu vya chuma vilivyo chomoza, minara ya simu, miti mirefu, milima, magorofa, nguzo za umeme vyote huwa vya kwanza kufikiwa na umeme wa radi kwa URAHISI kabla haijatua chini ya ardhi, ndo maana kitaalamu haushauriwi kuegemea hivyo vitu pindi mvua inaponyesha unaamua kukimbia sehemu ya tambalale ya ardhi mbaya zaidi unanyeshewa mvua na maji yanapitisha umeme wakati radi ikipiga kabla ya kuifikia ardhi itaanzia kwenye ubongo wako au eti unajikinga na mvua unaenda kuegamia mti kitakachokukuta watu wasio na elimu watadai umetumiwa radi na wachawi kumbe wewe ndo umeenda kukaa kwenye njia ya radi inapopita ili ishuke aridhini kwanini isipite na wewe..

Ukisoma Physics au sayansi kwa ujumla haya ma imani mengine mtaani utagundua ni ujinga flani seriuos watu wana aminishana sana na kurithishana kizazi na kizazi....
 
Nijitahidi kuelezea kwa lugha rahisi:

Kujua kama kuna aina fulani ya nguo au rangi fulani inaweza kuvuta radi, yabidi ufahamu radi ni nini.

Nadhani kila mmoja amewahi kuchukua plastic au kitana cha plastic, akakisugua sana kwenye nywele zake, halafu upeleke plastic hiyo kwenye karatasi. Plastic itaivuta karatasi, na baadaye huachia. Kitendo hiki nakifananisha na radi inavyotengenezeka.

Kwenye anga, mawingu husuguana, msuguano huo huwa ni mkubwa kiasi cha kutengeneza kiwango kikubwa sana cha charge za umeme, negative na positive. Msuguano huo husababisha joto kali mpaka kufikia nyuzi joto sentigredi 25,000. Ufahamu kuwa chuma huyeyuka kwenye nyuzi joto sentigredi 800 tu.

Charge hizi zinafuata kanuni ya umeme yaani wakati wote zinatafuta low potential energy ambayo ni ardhi. Zinashindwa mara mpoa kwenda ardhini kwa sababu hewa ni poor conductor. Lakini charge hizi zinapofikia kiwango kikubwa sana, na kusababisha joto kali, hewa hulazimishwa kuwa conductor, na kuzipitisha hizi charge kuelekea ardhini, ambayo ni low potential area. Kwa vile hewa ni poor conductor, charge hizi zinaposhuka wakati wote hutafuta conductor iliyo bora zaidi kuliko hewa. Kama kuna jengo refu, mti mrefu, mnara mrefu, basi zitaamua kupitia hapo, na kwa vile charge hizi zimebeba joto kubwa, zikipitia kwenye mti mrefu, utachanika na kukauka, kama mtu alisimama chini ya huo mti, naye atakaushwa (kumbuka kanuni ya umeme: katika kwenda kwenye low potential area, always seeks the shortest path possible). Kama binadamu umesimama kwenye uwanda wa wazi, hakuna miti wala kitu kilicho kirefu kukuzidi wewe, shortest path kufikia ardhi itakuwa ni kupitia kwako, na hapo ndiyo tunasema, mtu amepigwa na radi.

Kanuni ya charge, kama ilivyofanyiwa kazi na mtaalam Faraday, charge hazipenyi kwenye sphere, zitaizunguka tu. Ndiyo maana huwezi kusikia gari limepigwa na radi. Kwa sababu lenyewe ni kama sphere, charge zitazunguka nje, hazitapenya ndani, na kwa vile tairi ni mpira, ambao ni non-conductor, basi gari haitakuwa the shortest path ya kupeleka charge za umeme ardhini. Kipindi cha mvua, kama unaendesha gari, na kulikuwa na radi, usipende kulishika gari kwa nje wakati unashuka, kunaweza kuwa na charge za umeme wa radi ambazo hazijapata njia ya kwenda ardhini, ukishika zitapitia mwilini mwako, utapata mshtuko, lakini hazina uwezo wa kuua kwa sababu huwa ni kiasi kidogo.

Kanuni nyingine ni charge hizi kupenda sharp point, yaani ukiwa na chuma kipana na kingine kimechongoka, charge za radi zitapitia kwenye kile chuma kilichochongoka. Ndiyo maana ile mitego ya radi kwenye majengo marefu ni chuma chembamba kilichochongoka kitakachozidi kidogo urefu wa jengo, na lazima kiwe conductor nzuri. Radi kwa kutafuta shortest distance na kanuni ya kutafuta sharp point, lazima ipige hapo.

Radi ni discharge ya umeme kutoka kwenye atmosphere, hazina macho wala hazina uhai, haziwezi kutambua rangi ya kitu. Hivyo, hakuna rangi ambayo inavuta radi.

Mnyama kondoo hawezi kupigana na radi, bali mwanga mkali wa radi humshtua. Kondoo kama ilivyo kiumbe kingine chochote, akiwa kwenye njia ya radi inapoelekea ardhini, naye atapigwa na kufa. Huko Georgea, Marekani, kondoo wapatao 500 walipigwa na radi na wote kufa kwa pamoja.
Asante sana mkuu umedadavua vyeeeema
 
Inategemea uko wapi na umekutana na radi ya aina gani, kama ni hii ya kisayansi tunayoijua wote sawa, ila kama ndio uko nyanda za juu kusini na ukakutana na ile radi ya kichawi, unaweza usipate huo muda wa kujuta kwamba hatukwambia, shauri yenu mengine msijaribu hasa mkiingia anga za watu! Iteni tu uzushi
Kuna watu hupigwa rad kiangazi jua kali kichiz
 
Ngoja nikupe hii elimu kifupi sana itakufanya uachane na hizi imani, Iko hivi mawingu ya mvua kwa juu ni positive charged (+) na kwenye kitako/base yake yaani uanvyonyanyua kichwa chako juu kuyatazama mawingu juu ndo chini yake (base/kitako cha mawingo) so hii base ya chini ya mawingu ni negative charged in nature (-) sasa mkuu dunia yetu...
Ila kwann maradi hutokea kipind cha mvua
 
Myths that kill

The colour red doesn’t attract lightning, and covering the mirrors in a house won’t make a difference. Syringa trees aren’t more strike-prone than other tree species of similar height, and a tyre on the roof won’t drive lightning away.

But these won’t make you less safe. It is other myths that can kill.
The thick rubber soles of hiking boots won’t electrically isolate you from the ground and keep you safe — they’ll just melt on to your feet if you’re struck.
It’s the metal enclosure and not the tyres of a car that makes being inside one safe. The forces involved are far too powerful to be stymied by such small elevation — so riding a motorcycle in a thunderstorm is a very bad idea.

The beliefs most likely to kill, though, are the supernatural.
“Many South Africans believe some people can control lightning,” says Estelle Trengove, a Wits lecturer who has worked in the field. “Sometimes the belief is that natural lightning won’t kill you but that man-made lightning can be sent to target you.”
That is where muti buried around the house or rubbed on to the skin comes in. Though harmless in itself, the resulting sense of invulnerability doesn’t help. Also, if you think man-made lightning caused a death, it may seem a good idea to stop the person responsible.
Trengove is studying myths. She believes dismissing them as superstitious nonsense will achieve nothing.

Avoiding a strike
Ryan Blumenthal, a senior specialist at the forensic medicine department at the University of Pretoria, has conducted autopsies on the victims of lightning strikes, examined animals killed by lightning, written academic papers on safety precautions and spoken at schools and clubs about safety in thunderstorms. Yet he boils down all his experience to one catchy phrase: “When lightning roars, go indoors.

“Around the world lightning is the most consistent weather killer and the most preventable,” Blumenthal said. “There’s only so much you can do about a tsunami but with lightning some simple rules will keep you safe.”
The easiest rules to follow also dramatically reduce the risk of injury. Get out of the open, off or out of water and into a house or car with a full metal roof. Once inside, stay away from landline phones and anything plugged into a wall socket.
If you’re caught outside, things get more tricky. Stay well away from trees and anything tall. Get down from the tops of hills and ridge lines.
If you have to sit out a storm, resign yourself to getting wet and crouch down with your feet tightly together and no other part of your body touching the ground.

‘One moer of a bang’
To completely rule out being struck by lightning you need to go a little further. Until three decades ago you could be forgiven for constructing a nuclear reactor or ammunition dump, erecting a really tall copper pole next to it, and congratulating yourself on a job well done.
Then we found out about positive lightning. About 80% of all lightning jumps from cloud to cloud, never presenting a threat, and almost every strike that hits the earth is classic negative-downward, which seeks out the highest available point and adores lightning conductors. A very small number of strikes, however, are positive lightning.

“Sometimes you can hear it,” said Ian Jandrell, a Wits lightning professor. “It goes ‘bang’, ‘bang’, ‘bang’, ‘bang’, ‘bang’, then it goes quiet — and then there’s one moer of a bang. That’s positive lightning, which comes towards the end of the storm when the negative charge has been depleted.”

Positive lightning breaks the rules. It touches down where it pleases, ignoring masts and other high points. It is usually far more powerful and so causes more destruction.
The only way to protect against such strikes is expensive: enclose everything in a grid of interconnected conductors, preferably a tight one, then connect as much of that grid as you can to conductors buried deep in the ground. Then cower inside any time a cloud comes within 100km and you’re safe — at least until we learn something new about the nature of lightning.

Tags: Lightning Strike, MYTHS, Phillip De Wet, South Africa
 
Nijitahidi kuelezea kwa lugha rahisi:

Kujua kama kuna aina fulani ya nguo au rangi fulani inaweza kuvuta radi, yabidi ufahamu radi ni nini.

Nadhani kila mmoja amewahi kuchukua plastic au kitana cha plastic, akakisugua sana kwenye nywele zake, halafu upeleke plastic hiyo kwenye karatasi. Plastic itaivuta karatasi, na baadaye huachia. Kitendo hiki nakifananisha na radi inavyotengenezeka.

Kwenye anga, mawingu husuguana, msuguano huo huwa ni mkubwa kiasi cha kutengeneza kiwango kikubwa sana cha charge za umeme, negative na positive. Msuguano huo husababisha joto kali mpaka kufikia nyuzi joto sentigredi 25,000. Ufahamu kuwa chuma huyeyuka kwenye nyuzi joto sentigredi 800 tu.

Charge hizi zinafuata kanuni ya umeme yaani wakati wote zinatafuta low potential energy ambayo ni ardhi. Zinashindwa mara mpoa kwenda ardhini kwa sababu hewa ni poor conductor. Lakini charge hizi zinapofikia kiwango kikubwa sana, na kusababisha joto kali, hewa hulazimishwa kuwa conductor, na kuzipitisha hizi charge kuelekea ardhini, ambayo ni low potential area. Kwa vile hewa ni poor conductor, charge hizi zinaposhuka wakati wote hutafuta conductor iliyo bora zaidi kuliko hewa. Kama kuna jengo refu, mti mrefu, mnara mrefu, basi zitaamua kupitia hapo, na kwa vile charge hizi zimebeba joto kubwa, zikipitia kwenye mti mrefu, utachanika na kukauka, kama mtu alisimama chini ya huo mti, naye atakaushwa (kumbuka kanuni ya umeme: katika kwenda kwenye low potential area, always seeks the shortest path possible). Kama binadamu umesimama kwenye uwanda wa wazi, hakuna miti wala kitu kilicho kirefu kukuzidi wewe, shortest path kufikia ardhi itakuwa ni kupitia kwako, na hapo ndiyo tunasema, mtu amepigwa na radi.

Kanuni ya charge, kama ilivyofanyiwa kazi na mtaalam Faraday, charge hazipenyi kwenye sphere, zitaizunguka tu. Ndiyo maana huwezi kusikia gari limepigwa na radi. Kwa sababu lenyewe ni kama sphere, charge zitazunguka nje, hazitapenya ndani, na kwa vile tairi ni mpira, ambao ni non-conductor, basi gari haitakuwa the shortest path ya kupeleka charge za umeme ardhini. Kipindi cha mvua, kama unaendesha gari, na kulikuwa na radi, usipende kulishika gari kwa nje wakati unashuka, kunaweza kuwa na charge za umeme wa radi ambazo hazijapata njia ya kwenda ardhini, ukishika zitapitia mwilini mwako, utapata mshtuko, lakini hazina uwezo wa kuua kwa sababu huwa ni kiasi kidogo.

Kanuni nyingine ni charge hizi kupenda sharp point, yaani ukiwa na chuma kipana na kingine kimechongoka, charge za radi zitapitia kwenye kile chuma kilichochongoka. Ndiyo maana ile mitego ya radi kwenye majengo marefu ni chuma chembamba kilichochongoka kitakachozidi kidogo urefu wa jengo, na lazima kiwe conductor nzuri. Radi kwa kutafuta shortest distance na kanuni ya kutafuta sharp point, lazima ipige hapo.

Radi ni discharge ya umeme kutoka kwenye atmosphere, hazina macho wala hazina uhai, haziwezi kutambua rangi ya kitu. Hivyo, hakuna rangi ambayo inavuta radi.

Mnyama kondoo hawezi kupigana na radi, bali mwanga mkali wa radi humshtua. Kondoo kama ilivyo kiumbe kingine chochote, akiwa kwenye njia ya radi inapoelekea ardhini, naye atapigwa na kufa. Huko Georgea, Marekani, kondoo wapatao 500 walipigwa na radi na wote kufa kwa pamoja.
Mkuu nataka hii post isinipotee nafanyeje nataka niisome mara nyingi zaidi😍😍😍
 
Vipi kuhusu matumizi ya simu wakati mvua inanyesha! Nayo ina ukweli kuwa ukitumia simu wakati wa mvua utapigwa radi?!
 
Back
Top Bottom