Msanii wa muziki wa bongo fleva ambaye anafanya
poa katika anga za kimataifa Vanesa mdee,
amefunguka sababu ya yeye kupenda kuvaa nguo za
nusu utupu.
Akiwa kwenye kipindi cha Friday Night Live
kinachorushwa na East Africa Radio na EATV,
Vanessa Mdee amesema anapenda kuvaa mavazi
hayo ambayo hayakubaliki kwa jamii, kwa sababu
anatangaza brand yake, na hatimaye impe dili la
matangazo kwa wabunifu wa mavazi.
“Ukweli ni huu, wasanii for a long time in the past,
wasanii wa kitanzania hawajajua na kutambua brand
yao, mi brand yangu mi nataka ndani ya miaka miwili
napigiwa simu na Balmain, na Louis Vuitton, nataka
designers wakubwa wa dunia wanitumie kutangaza
bidhaa yao kwa sababu wanaamini nina brand yangu
kubwa na zinaendana, so nna malengo , na if im
gonna offend anybody im sorry”, alisema Vanessa
Mdee.
Vanessa Mdee ambaye kwa sasa ameachia video
yake mpya ya Niroge, amesema ana mipango ya
kufika na kutambulika dunia nzima katika kazi zake za
muziki, kama alivyochora ramani ya dunia kwenye
mkono wake.