Babu yangu alitusimulia historia ya Vita vya Kwanza ya dunia mwaka 1914 hadi 1918. Alisema wakati wa vita kati ya Mjerumani na Mwiingereza, wanaume wote ambao walikuwa na umri wa kwenda vitani walikuwa mapema alfajiri wanatoka kwenda mafichoni maporini. Ikawa askari wa Kijerumani wakija kusaka vijana wa kwenda vitani, wanakuta wanawake na watoto bila wanaume.
Askari wa Kijerumani baada ya kuona hivyo, wakabuni mbinu ya kuwakamata wanawake na watoto na kuwapeleka kwenye makambi yao.
Babu yetu akatwambia, siku moja waliporudi usiku wakaambiwa wanawake na watoto wamechukuliwa na askari. Kwa njia hiyo ikabidi babu zetu wajitokeze na kwenda kujisalimisha kwa askari wa Kijerumani ili kuwakomboa wanawake na watoto waliokuwa mateka.
Swali. Je, mbinu iliyotumika kumteka dada yake Humphrey Polepole itamfanya bwana Polepole ajisalimishe kwa watekaji ili kumkomboa dada yake?