Ikiwa Leo ni siku ya nne, najaribu kuingia kwenye system ya "NACTVET" Kuomba "AVN NUMBER" lakini sifanikiwi licha ya kuwa nimejisajili, ila system haijanipa nafasi ya kutengeneza password, na hata siwezi kuingia kabisa, na mbaya zaidi mfumo unload tu Wala hata haufunguki,
Ikiwa zimebakia siku tatu tu kufungwa Kwa dirisha la application vyuoni, na mkopo pia hivi karibuni watafunga, lakini NACTVET hawaoneshi ushirikiano kabisa, namba. Licha ya kuwa wameweka namba za mawasiliano lakini haipatikani na baadhi hazipokelewi hata moja, na tukituna notifications kwenye email yao, hawatusaidii!
N.B. Ni vyema wakwasaidia wanafunzi wanaopata changamoto kama hizo na baadhi, kwani hii inasababisha kurudisha maendeleo ya wengi nyuma, na taifa Kwa ujumla.