Kuvimba matezi (tonsils) shingoni

Loftins

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2017
Posts
10,485
Reaction score
13,693
Habari wakuu, samahanini kwa maelezo yangu marefu ila sina jinsi inabidi nieleze yote.
.
Naishi na mpwa wangu ana umri wa miaka 17 yuko kidato cha nne huyu bwana mdogo ana tatizo la kuvimba tezi za shingo hili tatizo limemuanza mwaka wa jana miezi ya mwishoni kwa wakati huo wala hakunieleza alitumia dawa (antibiotics) kikaisha kilikuwa upande wa kushoto wa shingo chini ya sikio.
.
Sasa kikamrudia tena hiki nachokieleza hapa ni kwa mujibu wa maelezo yake baada ya kunieleza hili tatizo kama wiki tatu zilizopita, anasema toka kimrudie huwa kinafifia tu ila hakiondoki na ameahatumia antibiotics mara mbili, cha kushangaza kikaongezeka kingine karibu na koo kikubwa zaidi hivi vyote havina maumivu hata kidogo.
.
Ikabidi nimepeleke duka la dawa (pharmacy) akapatiwa antibiotics tena kama aina mbili hivi za kumeza siku tano havikuisha yani cha upande wa pembeni wa shingo hakionekani kabisa mpaka umguse ila cha chini ya shingo akinyanyua kichwa juu kinaonekana.
.
Jana kimemtokea kingine tena cha mara hii hata mimi niliwahi kukipata kina maumivu ukikishika katika kufukunyua mitandaoni nikaona maandiko mengi ikiwemo uwezekano wa HIV ikabidi nikampime mpwa bila yeye kujua kijihospital cha mtaan hapa yuko vizuri tu.
.
Kinachonishangaza dogo akichana nywele zinakatika sehemu ya mbele kama anataka kupata kipara yani hazikatiki nyuma, katikati wala pembeni ni mbele tu na anaongezeka uzito hadi tunamshangaa katoka 64-73Kg anakula sanaa.
.
Anasumbuliwa na kiungulia sanaaa akila maharage na ndio mboga yake pendwa ni mbaguzi sana wa vyakula pia anatatzo la kifua kinambana hii ni kwa sababu ya pumu japo hatujathibitisha ila tunahisi kwa sababu ipo kwa bibi yake mzaa mimi na hawapatani na vumbi, perfume wala chenye harufu kali
.
Ana historia ya kuumwa gono haya alimueleza mfamasia yotee alafu wala haonyeshi dalili za kuumwa yuko kawaida kabisa ila ana hofu
Msaada wakuu Sky Eclat na wangine woooote
 
Akachek HIV
Nilimcheki mkuu bila yeye kujua yuko vizuri tu, mfamasia alisema huenda ni kiungulia kinachomsumbua kuna wakati vinasababisha hadi vimbe shingoni alisema ni reflex arc kama sijakosea
 
Mkuu mie pia naomba kufatilia hapa.

Nimuhanga wa Tonsils mpka saivi situmii vitu baridi na matembea na scaf shingoni kukwepa Baridi.

Nadhani dawa ni kujikinga na baridi.
 
Mkuu mie pia naomba kufatilia hapa.

Nimuhanga wa Tonsils mpka saivi situmii vitu baridi na matembea na scaf shingoni kukwepa Baridi.

Nadhani dawa ni kujikinga na baridi.
Huenda ni kweli boss kwa sababu kuna rafiki yangu nae zimeanza kumsumbua.
.
Tatizo huyu dogo hayamuishi sasa sisi zamani tulizoea ya kinywani tunaingiza mamiswaki tunajisugua na chumvi yanaisha😂
 
Wakuu karibuni kwa msaada 🙏
 
Tonsillitis

An inflammation of the two oval-shaped pads of tissue at the back of the throat.

Tonsillitis is usually caused by a viral infection but can be from a bacterial infection.

Symptoms include sore throat, difficulty swallowing and tender lymph nodes.

People may experience:
•Pain areas: can occur while swallowing or in the ear

•Whole body: chills, fatigue, fever, or malaise

•Nasal: congestion or runny nose

•Speech: impaired voice or laryngitis

•Also common: bad breath, enlarged neck lymph nodes, excess salivation, mouth breathing, poor appetite, pus, snoring, sore throat, swollen tonsils, or tender lymph nodes

Treatment
Treatment can range from home-care remedies to surgical removal.

=>Self-care
•Tea with honey
Soothes sore throats.

•Salt water gargle
Soothes sore throats.

•Throat lozenge
Soothes sore throats.

=>Medications
•Nonsteroidal anti-inflammatory drug
Relieves pain, decreases inflammation and reduces fever.

•Analgesic
Relieves pain.

•Penicillin antibiotic
Stops growth of or kills specific bacteria.

•Antibiotics
Stops the growth of or kills bacteria.

=>Surgery
•Tonsillectomy
Surgical removal of the tonsils..

=>Specialists
•Otolaryngologist
Treats ear, nose and throat disorders.

=>General Practitioner (GP)
•Prevents, diagnoses and treats diseases.

Source: Google
 
Shukrani sana mkuu mwifwa 🙏
 
Mchawi wa kumtibu tonsilitis kwa antibiotics wako watatu ambao ni nyoko balaa

Ampiclox, phenoxmethlypenicillin(pen V) na microlides zote haswa erythromycin.
 
Mchawi wa kumtibu tonsilitis kwa antibiotics wako watatu ambao ni nyoko balaa

Ampiclox, phenoxmethlypenicillin(pen V) na microlides zote haswa erythromycin.
Zinatibu hata chronic mkuu?
 
Mwambie dogo kama ana tabia ya kutumia vitu vya baridi aache mara moja,maji,ice cream,soda za baridi hapa namaanisha zilizotoka kwenye fridge,hata matunda ya baridi asitumie.Kingine ni hali ya hewa kama anaishi sehemu zenye baridi sana lazima yatakuwa yanajirudia,aepuke pia kulala dirisha wazi au upande ambao uko karibu na dirisha hasa la wavu kwani wakati wa usiku kuna hewa nyingi ya ubaridi inapenya na inaweza ikawa ni chanzo..
 
Ni kweli mkuu tunaishi sehemu yenye baridi sana nyakati za usiku, lakini ndio akatike nywele kwa mbele,aongezeke uzito kwa kasi maana dogo hadi kapata kakitambi wakati huwa ni kembamba na anafukia msosi balaa😂
.
Huenda viungulia navyo vikawa ni sababu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…