Loftins
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 10,485
- 13,693
Habari wakuu, samahanini kwa maelezo yangu marefu ila sina jinsi inabidi nieleze yote.
.
Naishi na mpwa wangu ana umri wa miaka 17 yuko kidato cha nne huyu bwana mdogo ana tatizo la kuvimba tezi za shingo hili tatizo limemuanza mwaka wa jana miezi ya mwishoni kwa wakati huo wala hakunieleza alitumia dawa (antibiotics) kikaisha kilikuwa upande wa kushoto wa shingo chini ya sikio.
.
Sasa kikamrudia tena hiki nachokieleza hapa ni kwa mujibu wa maelezo yake baada ya kunieleza hili tatizo kama wiki tatu zilizopita, anasema toka kimrudie huwa kinafifia tu ila hakiondoki na ameahatumia antibiotics mara mbili, cha kushangaza kikaongezeka kingine karibu na koo kikubwa zaidi hivi vyote havina maumivu hata kidogo.
.
Ikabidi nimepeleke duka la dawa (pharmacy) akapatiwa antibiotics tena kama aina mbili hivi za kumeza siku tano havikuisha yani cha upande wa pembeni wa shingo hakionekani kabisa mpaka umguse ila cha chini ya shingo akinyanyua kichwa juu kinaonekana.
.
Jana kimemtokea kingine tena cha mara hii hata mimi niliwahi kukipata kina maumivu ukikishika katika kufukunyua mitandaoni nikaona maandiko mengi ikiwemo uwezekano wa HIV ikabidi nikampime mpwa bila yeye kujua kijihospital cha mtaan hapa yuko vizuri tu.
.
Kinachonishangaza dogo akichana nywele zinakatika sehemu ya mbele kama anataka kupata kipara yani hazikatiki nyuma, katikati wala pembeni ni mbele tu na anaongezeka uzito hadi tunamshangaa katoka 64-73Kg anakula sanaa.
.
Anasumbuliwa na kiungulia sanaaa akila maharage na ndio mboga yake pendwa ni mbaguzi sana wa vyakula pia anatatzo la kifua kinambana hii ni kwa sababu ya pumu japo hatujathibitisha ila tunahisi kwa sababu ipo kwa bibi yake mzaa mimi na hawapatani na vumbi, perfume wala chenye harufu kali
.
Ana historia ya kuumwa gono haya alimueleza mfamasia yotee alafu wala haonyeshi dalili za kuumwa yuko kawaida kabisa ila ana hofu
Msaada wakuu Sky Eclat na wangine woooote