Kuvuja mitihani ya Form four kila mwaka NECTA na waziri wa elimu wajiuzulu!

Kuvuja mitihani ya Form four kila mwaka NECTA na waziri wa elimu wajiuzulu!

Songambele

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2007
Posts
4,710
Reaction score
2,587
Leo imeripotiwa kuwa mtihani wa Mathematics kwa Form IV umehairishwa kufanyika leo kwa sababu umevuja na utafanyika jumatatu ijayo. Hii ni habari mbaya kwa vijana waliojiandaa kufanya mtihani leo kutokana na uzembe wa wizara ya elimu na baraza la mitihani kushindwa kutimiza wajibu wao wa kulinda mitihani.

Hii sio poa na waziri wa elimu anawajibika kujiuzulu akifuatiwa na uongozi wa baraza ili kuruhusu uchunguzi zaidi kwa nini hawa jamaa bado wanatoa mitihani. Utaratibu wa huu wa mithani una walostisha sana vijana ambao wasingeweza kupata hata huo mtihani fake wenyewe.

Inawezekana pia ushindani wa shule uliopo sasa unaweza kuwa ndio kichocheo zaidi kila mtu anataka mtoto wake au shule yake iwe ya kwanza hata kama haina uwezo ukizingatia wasimamizi wa mitihani wako corrupted lazima mtihani uvuje. Lakini hii sio sababu pekee manake na walimu pia wanahusika kuvujisha.

Miaka yote paper inavuja na business as usual sio poa.
 
Songambele nakubaliana na wewe 100% nadhani hawa NECTA wana matatizo haiwezekani mara results slip zimeibwa sasa tena mitihani imevuja. There must be something wrong pale nadhani hata Dr. Ndalichako anatakiwa akae pembeni maana inaonekana katika hiki kipindi cha utawala wake hali imekuwa mbaya....Go Maghembe kazi umechemsha.
 
My Take on this

Wingi wa walimu ambao hawana vipato vya kutosha,migogoro ya wizara ya elimu na walimu,wizara nzima kuwa iliyo jaa rushwa.

1. Kuna walimu wengi sana...ambao...kwa sasa hawana mahala pa kushika...na hata wito wenyewe hawana wa kazi..kwa kuwa hawakuwa na option nyingine ya kupata kazi wakaamuwa kwenda kwenye ualimu...sasa ndio matokeo yake.
2.Migogoro mingi kati ya wizara na walimu...mara haiwatambui..mara hawajui vituo vyao vya kazi.
3.Mabadiliko na mchanganuo wa mgawanyo wa kazi baada ya wizara kutenganisha baadhi ya majukumu na kuyagawa kwenye wilaya husika...
4.Kutokuwa na vitendea kazi..na maeneo mazuri ya kazi...
 
Pole sana Dr. Joyce Ndarichako kitumbua chako kinaingia mchanga sasa. Ninavyofahamu mimi, pamoja na matatizo ya walimu ambayo tunaya-link- na kuvuja kwa mithani, ifahamike wazi kuwa sio walimu wote wanahusika moja kwa moja kushika mitihani. Kama ni shule ya secondary only the headmaster anahusika. Kama ni Pale NECTA kuna kitengo cha mitihani na kinawafanyakazi wake, hali kadhalika kwa wanaosafirisha mitihani wanafahamika. If NECTA is serious, stil can trace where the problem originated na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria. Walimu walio wengi wanaiona mitihani siku ya kufanya mithani yenyewe. .
 
Hapa suala si kilichopelekea mtihani kuvuja,tunachotaka hapa kila aliyekuwa kwenye chain ya mtihani huu anapaswa kujiuzulu,akae pembeni.If you can't do it,somebody can.Mpaka hapo wadogo zetu wameshayumba,si unajua wengine hesabu tunasomea D.Masikini zile kanuni zote zilizokuwa zimeegeshwa,ndo basi tena.You know what it takes kuziegesha tena!
 
hizi garama za kuandaa hilo somo upya ni za nani? kwa nini watu hawawajibiki? umakini mbona haupo kwenye suala nyeti kama hili? mitihani inavuja na vyeti vinafojiwa. kazi imewashinda
 
=FUGWE;297368]Pole sana Dr. Joyce Ndarichako kitumbua chako kinaingia mchanga sasa.
???????????
Ninavyofahamu mimi, pamoja na matatizo ya walimu ambayo tunaya-link- na kuvuja kwa mithani, ifahamike wazi kuwa sio walimu wote wanahusika moja kwa moja kushika mitihani. Kama ni shule ya secondary only the headmaster anahusika. Kama ni Pale NECTA kuna kitengo cha mitihani na kinawafanyakazi wake, hali kadhalika kwa wanaosafirisha mitihani wanafahamika. If NECTA is serious, stil can trace where the problem originated na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria. Walimu walio wengi wanaiona mitihani siku ya kufanya mithani yenyewe...
mtihani umevujia baraza sio shuleni kwa shule za dar mitihani iasambazwa siku hiyo kwa hiyo mkuu wa shule halali na mtihani.Huu mtihani nasikia umevuja siku kadhaa sio leo au jana....
kama vyeti vinapatikana baraza sembuse mtihani nani asiependa pesa pale NECTA na mishahara yao midogo
 
Vijana wameyumbishwa sana hasa wale walikwisha kujiandaa kwa hesabu...kuna wale ambao...ndoa yao ilisha katika na hesabu toka shule ya msingi...so walikuwa wanasema bora tumalize twende kwenye uwezo wetu.

Sasa hapa inasemekana itakuwa tena tarehe 20 hivi...sasa muda wote huo wanasubili...
Matatizo yapo ingawa hayahusiki moja kwa moja ila kwa kweli yanahitajika kuwa sorved.
 
Kwenye NCHI iliyotamalaki RUSHWA na UFISADI kila kitu kinawekwa sokoni au mnadani. Ni pesa yako tu!
 
mna hakika huo mpya hautavuja? Kwa kuwa kilichovujisha huu wa sasa kipo basi na huo utavuja pia,kama si hesabu basi ni masomo mengine. Kwa sababu jamaa aliowauzia hiyo mitihani watadai fedha zao na jamaa atawapoza kwa kuwaibia mtihani mwingine,iwe pale NECTA au huko shuleni kwenyewe.
 
Ni aibu kila mwaka tunaongelea suala hilo hilo la kuibiwa mitihani. Baraza la mitihani na wizara ya elimu inaonyesha uzembe wa hali ya juu. Uchunguzi wa kina ufanyike ili kunusuru vijana wetu kwa kukosa kukosa kufanya mtihani wa hesabu kwa muda uliopanga. Hii inaharibu mipango ya wanafunzi.
 
Taarifa zilizopo ni kuwa mitihani mitano(civics,maths,physics,french na hist)imezagaa kona za nchi.

Hii ni zaidi ya fedheha kwa kweli.Suala siyo kujiuzulu tu wala kufukuzwa kazi.Kuna chain ndefu sana ya wezi wa mitihani.Pale NECTA kuna kitengo cha printing,quality assurance na control ya strong room.

Nijuavyo mimi ni kuwa wahusika wa printing na strong room huwekwa chini ya ulinzi wa hali ya juu na polisi wetu na maofisa wa juu wa NECTA.Hupekuliwa mpaka kwenye kucha wakiwa wanatoka ndani ya chumba husika.Chakushangaza maofisa na polisi wanaosimamia zoezi huwa hawapigwi search.Hapo panaweza kuwa na mazingira ya kutia shaka.

Lazima tudhibiti hali hii la sivyo tunazidi kufuga ugonjwa mbaya
 
Taarifa zilizopo ni kuwa mitihani mitano(civics,maths,physics,french na hist)imezagaa kona za nchi.

Hii ni zaidi ya fedheha kwa kweli.Suala siyo kujiuzulu tu wala kufukuzwa kazi.Kuna chain ndefu sana ya wezi wa mitihani.Pale NECTA kuna kitengo cha printing,quality assurance na control ya strong room.

Nijuavyo mimi ni kuwa wahusika wa printing na strong room huwekwa chini ya ulinzi wa hali ya juu na polisi wetu na maofisa wa juu wa NECTA.Hupekuliwa mpaka kwenye kucha wakiwa wanatoka ndani ya chumba husika.Chakushangaza maofisa na polisi wanaosimamia zoezi huwa hawapigwi search.Hapo panaweza kuwa na mazingira ya kutia shaka.

Lazima tudhibiti hali hii la sivyo tunazidi kufuga ugonjwa mbaya

Hii hatari sasa kuna haja gani ya kuendelea kufanyika kwa huu mtihani?unakosa maana ya kuwa mtihani!Hii nchi hii tutakuwa vihiyo hadi mwisho wa dunia kama mambo yenyewe ndo Haya
 
wa kuwajibika ni walimu na wakuu wa shule, Mkuu wa NECTA awajibishwe kwa kitu gani? Kuna haja ya kuunda tume ili ichunguze tusihukumu kwanza. Labda halikuwa hajui kinachotokea hadi amesoma kwenye vyombo vya habari.
 
Jamii yetu JF inclussive imeshindwa kuokoka kwenye hili suala la double standards akikosea EL, RA et al., wanapigiwa kelele za kuwajibishwa, kwa NSSF, NECTA et al., hamna LOL.
 
wa kuwajibika ni walimu na wakuu wa shule, Mkuu wa NECTA awajibishwe kwa kitu gani? Kuna haja ya kuunda tume ili ichunguze tusihukumu kwanza. Labda halikuwa hajui kinachotokea hadi amesoma kwenye vyombo vya habari.

Mkkj kumbe ndo ulivyo!kumbe mkurungezi wa NSSF awajibike why wakati kuna kina;;;;;;;;;;!Pia why tusisubiri uchunguzi kabla ya kumuhukumu Bwana mkubwa wa NSSF?
 
Mkkj kumbe ndo ulivyo!kumbe mkurungezi wa NSSF awajibike why wakati kuna kina;;;;;;;;;;!Pia why tusisubiri uchunguzi kabla ya kumuhukumu Bwana mkubwa wa NSSF?

First Lady,

Inaonekana hukumuelewa MKjj...ameongea kimafumbo hapo.....
 
Nimepiga simu kwa mwalimu mkuu wa St Mathew, Kongowe, ambako kijana wangu nae anafanya mtihani huko anasema kilichofanyika ni mtihani wa hesabu kuahirishwa. Utafanyika 20.10.2008. Akasema sio kweli kuwa mitihani imeibiwa. Sijui kama anasema kweli au vipi!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kuna thread mbili kuhusu suala hili. Naomba Moderator aziunganishe ili twende na mtiririko mmoja
 
Back
Top Bottom