Kuvunjika kwa ndoa yake: Mzee Majuto aitwa BAKWATA...

Kuvunjika kwa ndoa yake: Mzee Majuto aitwa BAKWATA...

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
MAJ.PNG


SIKU chache baada ya ndoa ya supastaa wa vichekesho Bongo, Amir Athuman ‘Mzee Majuto’ kuvunjika, mke aliyeachika amekimbilia Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) kutoa malalamiko yake, Amani liko mbele kukuhabarisha.

Rehema Omar (20) ndiye mke aliyeachwa na Mzee Majuto, Septemba 14, 2013 alikimbilia Makao Makuu ya Bakwata Wilaya ya Kinondoni yaliyopo Hananasif, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa msichana huyo, mambo aliyoyazungumza kwenye ofisi hiyo ni matatu, kwanza kutopewa talaka baada ya kuachika.

Akasema akimuuliza Mzee Majuto kuhusu talaka yake anamwambia amempa mwanamke mmoja aitwaye Rehema amfikishie, akahoji: “Kwani huyo Rehema ndiye aliyenioa?”

Pili, akasema wakati anakaribia kufunga ndoa, mzee huyo alimwachisha kazi mahali na pia alimhamisha kwenye chumba alichopanga.

Tatu, akasema kutokana na hayo yote anaomba alipwe fidia ya fedha kwa sababu ya usumbufu alioupata.

Rehema akasema kutokana na malalamiko yake, viongozi wa Bakwata walimpa barua ya kumfikishia Mzee Majuto yenye kichwa cha habari cha WITO.

MAJ1.PNG


Mzee Majuto anatakiwa kufika bila kukosa kwenye ofisi hizo, Septemba 23, mwaka huu ambayo itakuwa Jumatatu ili shauri lake na mwanamke huyo lizungumzwe.

Juzi, Amani lilimpigia simu Mzee Majuto lakini muda wote iliita bila kupokelewa.

Toleo la gazeti hili lililopita, tuliandika ukurasa wa mbele habari yenye kichwa; NDOA YA MZEE MAJUTO YAVUNJIKA. Kwenye utetezi wake, mzee huyo alisema alimwacha mwanamke huyo baada ya kugundua hajatulia.
 
ndoa yenyewe alifunga ndani ya mwezi mtukufu wa ramadhan. ilo ni kosa nafikiri.
 
Mtani wangu mzee majuto wasikutishe,utakaa na mtu kiruka njia? Kuna dada wa kinyamwezi anakufaa sana
 
Mh jamani ingawa ng'ombe hazeeki maini, lakini hii ni too much mke 20yrs mme 65yrs
 
hili zee nalo,unaoa mjukuu wako hata hayo mapenz mnafanyaje, walidanganye tu
 
dogo dogo,,, HAPENDWI MTU HAPA,,,, PESA TWALA KWA MAJUTO MAPENZI MOTOMOTO NJE YA NDOA KWA AGEMATE
 
babu amejitakia anaoa katoto si majanga tu kumbe kuigiza kunajenga mazoea?
 
ni kosa kivipi,,hebu toa muongozo,,kufunga ndoa ramadhan makosa yake yanakujaje!!?
 
Haka katabia sasa kanakua wazee wa miaka kuanzia 50 na wanaokaribia kustaaf kwa kuwa wana vihela flani wanawavamia vidada ambavyo hata mtoto wake wa mwisho mkubwa aibusana hii dunia inaenda wapi mi naamini yesu anarud punde mana ni aibu tupu zimejaa mitaani
 
kumbe kuigiza mambo mengine ni uhalisia wa mtu ,katika filam nyingi anazoigiza mara nyingi anakuwa na hivi vidada kumbe mwisho inakuwa kweli, sijui huyu ni mke wake w angapi?
 
Wazee wenye urafi wenyewe wanasema they want to die while smilling.
 
Ana haki na wenye wivu wajinyonge. What is age if not just numbers. Mzee Majuto amefanya kosa gani mbele ya Mungu nyie mahakimu bandia.If you dont have cash like Mzee Majuto mtaishia kuwaita warembo mashemeji. Mbona Senator moja Nigeria mwenye umri wa miaka 62 kaoa mtoto wa kiaarabu mwenye umri wa miaka 16.
 
Back
Top Bottom