Kuwa kipa wa akiba katika timu ni kudumaza kiwango chako.

Kuwa kipa wa akiba katika timu ni kudumaza kiwango chako.

HOPEfull

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
1,882
Reaction score
2,313
Mi huwa sijui hawa makipa huwa wanacheza lini.Halafu unakubalije kuwa kipa wa akiba katika timu.Yaani usubiri hadi mwenzako aumie ndio na wewe ucheze.Hii ina maana umeshajiweka kuwa katika nafasi hiyo na umeridhika.
Mbona timu ziko nyingi kwa nini mtu usiende kikipiga katika timu zingine ambazo utakubalika kuwa kipa namba moja.Hii nafasi ya kipa wa akiba inatakiwa ifutwe kwa kuwa inadumaza kiwango cha mchezaji.
Basi afadhali ingekuwa wanapokezana kila baada ya mechi 2 au moja.
Mimi kwangu haaingii akilini kwenda uwanjani kama mtazamaji tu.Afadhali wachezaji wengine wa ndani wa akiba kuna siku wanaweza wakapata nafasi wakacheza.
Nashauri timu isitegemee kipa mmoja kila mechi wafanye kubadilishana ili kukuza kiwango.
Tulifanyie kazi .
 
Inaonekana una mihemko na haujui mpira. Hakuna anayesajiriwa awe golikipa namba 2 au 3 moja kwa moja bali ufanisi wako mazoezini na kwenye mechi utakufanya uanze au uishie kwenye mbao ndefu.

Pale Chelsea kuna mlinda lango wao anaitwa Kepa alisajiliwa ili aanze kwenye kikosi cha kwanza lakini ameishia kwenye mbao ndefu baada ya kuzidiwa ufanisi na mwenzio Mendy.

Kikubwa ni kupambana na si kulaumu kama wewe huku mitandaoni
 
Na sio lazima kipa namba moja aumie ndo apishe makipa wengine...


Ata kushuka kiwango au kushindwa kufit katika mifumo ya kocha kunaweza kufanya hao makipa wa akiba... Ambao unahisi wapo kushusha viwango vyao nao kuitumikia timu!

Na akuna nafasi isiyokuwa na presha katika mpira kama kuwa kipa wa akiba, hasa kocha akikuamini!
 
Haiwezekani ukae mwaka mzima unaenda uwanjani tu na kurudi.
 
Back
Top Bottom