Kuwa makini na Apps za Mikopo

MkopoWako
*
*KIAS*140180.000
MkopoWako:
UMEKUWA MTU WA SABABU NYINGI, UMEKUWA MTU USIYEONA UMUHIMU WA KULIPA DENI LAKO. WAPO WENGI WENYE SHIDA NA UHITAJI WA MUHIMU WANASHINDWA KUPATA MSAADA KWA SABABU YA UTAPELI NA UDHURUMAJI WAKO.

WAPO WAGONJWA WANATEGEMEA HIYO PESA ULIOKAA NAYO. ROHO NYINGI ZINATESEKA KWA SABABU YAKO.

MAUMIVU JUU YAO, VILIO VYAO NA MATESO YOTE WANAYOPITIA HAKIKA YATAKUJA JUU YAKO.

KUWA BINADAMU USIWE MNYAMA, WAONEE HURUMA BINADAMU WENZAKO WENYE SHIDA REJESHA PESA ILI WAPATE MSAADA.
AU TUPIGIE WADHAMINI WAKO TUWAELEZE JINSI UNAVOLETA USUMBUFU JUU YETU LABDA WATAKUSAIDIA KULIPA

N.B: LIPIA DENI LAKOO LA AWALI TUKUONDOLEE PENALT KWA ASILIMIA 100
 
JF WENGI MNAJIFANYA WAJUAJI MNA MAISHA MAZURI, KUMBE MAFUKARA MASIKINI OMBAOMBA HAMNA MAISHA HAMNA MBELE WALA NYUMA MMECHOKA NA KUCHAKAA...
Mnakopa hadi pesa za kununulia maandazi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ wapumbafu sana nyie
 
Nilikuwa nataka kukopa Branch na sijawahi kukopa nimedownload app Yao na kujisajiri ila nimeambiwa nisubiri baada ya siku 7 , je huwa inakuwa hivi hivi kwa mteja wa kwanza au ?
 
Uki jibiwa ni tag mzee
Nilikuwa nataka kukopa Branch na sijawahi kukopa nimedownload app Yao na kujisajiri ila nimeambiwa nisubiri baada ya siku 7 , je huwa inakuwa hivi hivi kwa mteja wa kwanza au ?
 
Shida ya hizi taasisi za kifedha haziaminiki. Binafsi nilikwazwa na Tala. Nikalipa, kumbe hawakopeshi tena. Nimewalipa 360,000 nikitaka nikope 300,000/-. Kuanzia hapo nilikopa branch na L-pesa nami nikawadhurum bora nijiunge na saccoss za mitaani pengine likitokea la kutokea unaweza kupata haki.
Ninavyokopa na kulipa basi ndio mzunguko wako wa kifedha huo ila walivyo nidhurumu tu Tala nikapata akili
 
Hao Pesa X/Cash X mimi pia nilitaka kuwalipa baada yakupitiliza siku, ila ghafla ikaja sms ya matusi na kejeli. Nilipandwa na hasira sana na nikaghairi. Sikuwalipa tena na wamehangaika hadi wamechoka maana ni mwendo wa block tuu. Hawana kauli nzuri hao washenzi
 
Wamempgia simu wife na sikumuweka kama wadhamini watakuwa wamepata wapi namba yake wamenshtua
πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£.

Mkuu unaogopa nini sasa,acha watakushtua zaidi hao.

Mimi nadhani kulog out na kutumia Vpn inaweza saidia wasipate data zako
 
Ila watu hamna huruma,meseji ya kinyonge kama hii bado unakomaa haulipi
 
Hivi hawa Tala wa Facebook ni kweli wanatoa mikopo? na kama ni ndio kwa nini hawataki kuongea nao, yaani wanataka uchat nao tuu na pia ukiwaambia uende ofisini kwao pia hawataki najiuliza kama hii kitu ni genuine na kama ni wezi basi wengi wanapigwa na serikali iko kimya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…