Kuwa makini na hizo kampani zako huko mtaani!

Hii inafikirisha sana nazungumzia mimi sio kupimwa yeye labda hakupina mwanzo ila maneno ya kuudhi ya mwanamke wake labda ndio yaliyochochea, hapo si umezungumzia makundi sasa kundi moja wapo ni mwanamke aliezaa nae unajua walizungumza nini kabla hajafanya tukio?
 
Kuna vitu vya kuwasingizia wanawake ila hili ni tamaa binafsi za kuwa tajiri
Sijasema kuwasingizia mkuu, hapo Actus Reus & Mens Rea lazima zitumike mpaka anatiwa hatiani yaan yale matukio yote jumuishi yaliyopelekea yeye kufanya tukio, sasa tukio moja wapo ni hilo la mazungumzo na mama wa mtoto unajua walizungumza nini na huyo mama wa mtoto kabla ya kufanya tukio? Maana hilo ni jambo la kutumia akili mtu mwenye akili sawa sawa hawezi akafanya hivyo hata km ameshawishiwa na mganga au mtu wa aina gani
 
Ndio maana nikarudisha mpira kwa kipa, labda mwanamke aliropoka maneno fulani yale ya kwanza huyu mtoto ana baba yake wewe sio baba yake usinibabaishe na chochote, mwamba akaona isiwe tabu akafungua bucha
Unajaribu kutafuta kitu cha kuhalalisha au kupooza huu unyama kwa sababu ambazo hata mimi sizijui. Hivi kuna uhalali wa kumfanyia mtoto yeyote namna hiyo?
 
Kupanga ni kuchagua kama angewin angepata machawa wajinga wajinga
Asingeweza ku-win kwa sababu huwezi kuwa tajiri kwa kuua mtoto wako. Hizi ni imani za kijinga kabisa na najua watanzania wengi wanaamini kwenye huu upumbavu. Ukiaona mtu anayeamini eg chuma ulete, hiyo ni nursery tosha ya kufikia kuamini kwenye ujinga kama huu.
 
Unajaribu kutafuta kitu cha kuhalalisha au kupooza huu unyama kwa sababu ambazo hata mimi sizijui. Hivi kuna uhalali wa kumfanyia mtoto yeyote namna hiyo?
Anajaribu kuleta hoja kama vile ni halali na Haina shida kama mtoto umebambikiwa sio wako
Awe wako asiwe wako bado haijustify kufanya huo unyama
 
Aisee
 
Lakini alikua anakaa na nani kwenye makundi? Nani alikua anamshauri? Ni dhahiri alikaa na mtu mwenye mafanikio akamwambia alimtoa kafara mwanae.
 
Anajaribu kuleta hoja kama vile ni halali na Haina shida kama mtoto umebambikiwa sio wako
Awe wako asiwe wako bado haijustify kufanya huo unyama
Ni kweli sister. Tena kisheria kufanya hivyo kwa sababu umeambiwa mtoto siyo wako ni mbaya zaidi kwa sababu motive ya kutenda unyama kama huu inajumuisha mambo mengi kulinganisha na mtu ambaye amekuwa brain washed na kuamini. All in all, huu ni unyama unaotakiwa kupingwa kwa adhabu kali kabisa.
 
Na huyu mhanga ni mkinga halafu mkazo wa iringa.huko kwao haya mambo yametaradadi sana.
Halafu watu wanawasifia Wakinga kuwa ni wachapakazi na watunza akiba. Kumbe utajiri wa masharti na makafara.

Tajiri ana gorofa Kariakoo lakini anakula kwa mama nitilie na kuvaa makambuga. Hayo mautajiri hayana faida yeyote
 
Intention to kill alikuwa nayo yeye actus reus bado inamuangukia yeye jamaa hata kama mens rea ni mkewe bado atakuwa suspect no 2! Hiyo ni malice aforethought!!
 
Watu wanataka maisha mazur Kwa njia za shortcut sio rahisi ivo
Waganga wanawaharibu sana vijana huko kwenye vijiwe Kila mtu anaile story wafanyabiashara wote wakubwa wanatumia ushirikina kufika walipo 😄

Hakuna mganga mkweli wote ni matapeli
 
Waganga wa kienyeji wamepotosha na kuharibia wengi sana
Wengine ni watu waliofanikiwa kwa njia za kificho na hawawezi kusema ukweli na kubaki kudanganya
Wengi wanafanya hivi kwa sababu huwa wanashindwa kutafakari kwa kina. Unaweza kwenda kwa mganga, akakumbia nenda kafanye kafara abc, na baada ya kufanya ukafanikiwa. Hii haimaniishi kuwa ile kafara ndiyo imekusaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…