JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Unapopanga kukutana ana kwa ana na mtu ambaye mmefahamiana kupitia mtandao ni vyema ukachukua tahadhari kwa kuwa sio kila mtu ni mkweli kwa namna anavyojitamulisha kwako, umri, jinsia, na nia yake kwako.
Ikiwa ni lazima kukutana naye, fanya utafiti kuhusu mtu huyo ili ufahamu ukweli wake, lakini hiyo haitoshi kumuamini.
Ukiamua kukutana naye, kamwe usiende peke yako, wajulishe wengine unakokwenda, ni vyema mkakutana mahali pa umma na uwe na simu yako ikiwa hewani.
Upvote
0