jouneGwalu
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 2,696
- 1,807
Kumekuwa na trend ya watu tunaoweza kusema ni content creators ambao wapo nje ya nchi wanatoa post/content mbali mbali kuhusiana na maisha ya ughaibuni.
Wengi wanazungumza umuhimu wa kujaribu fursa kwenye nchi zilizoendelea zaidi mfano wa nchi za ulimwengu wa Kwanza!
Binafsi nilikuwa Mpenzi wa content za namna hizo sababu kwanza kwa muda mrefu watanzania wengi waliotangulia kusafiri na kuishi nchi hizo walikuwa sio watu wa kutoa taarifa za maisha kwenye nchi hizo na pia kueleza options mbalimbali zinazoweza kupatikana ili kuwezesha mtu aliyepo Tanzania naye ajaribu kuzitumia kuingia kwenye nchi hizo.
Wakati sisi kwetu hali ilikuwa imejawa na ukimya kwa nchi za waafrika wenzetu kama Kenya na Nigeria, content za namna hiyo zilikuwa nyingi sana!
Ukiingia YouTube utapata contents nyingi mnoooo zinazoangazia masuala ya safari kwenda Ulaya na au Marekani au Australia na Japan, zikiwa zimeandaliwa na Wakenya na Wanaijeria.
Hivyo zilivyoanza content za watanzania ilikuwa kitu kizuri zaidi, Awali ilikuwa unawapata wakina EBM nadhani huyu amekuwa mkongwe zaidi japo alijikita zaidi na fursa kwa njia scholarship na DV lottery. EBM amefanya kazi kubwa na nzuri mnoooo.
Page yake ya YouTube ni itakufungua macho kwenye masuala muhimu sana ya namna ya kujipanga na safari.
Wakina EBM wakiwa ni waanzilishi wa kuweka content za safari kwa lugha ya kiswahili na kwaajili ya hadhira ya watanzania,
Baada ya mafanikio yao wakaanza kuibuka wengi sasa na baadae YouTube ikafurika hizo contents.
Kama nilivyosema awali sina upinzani na hizi content, Sanasana naunga mkono sababu binafsi nadhani Tanzania ni nchi ambayo raia wake tumejifungia sana ndani, Sio watu wa kupenda kusafiri na hata wachache wanaosafiri sio watoa taarifa za huko walipo (kuwe kuzuri au kubaya) tofauti na labda Wakenya na Wanaijeria.
Lengo la Uzi huu ni kutoa tahadhari na baadhi ya hawa content creators ambao wengine wamejigeuza wapanga safari; Kwamba wanakushawishi kuwa ukitaka kwenda kwenye nchi husika wanaweza kukusaidia kuomba Visa
Na tahadhari hii naitoa baada ya binafsi kukutana na mkasa wa hawa wapanga safari ambapo mwishoni nilijikuta nimepoteza hela nyingi sana na msaada wa huyo mpanga safari haukwenda kama alivyoahidi huku utendaji wake wa kazi ukiwa na uwalakini mwingi sana.
Hivyo unapowasikiliza na maneno yao mengi Baki kuwa na tahadhari;mKuna vitu jiridhishe kabla hujaanza kulipa hela ya kupangiwa safari
1. Awe na ofisi ya jina lake hapa Tanzania sio anadandia ofisi za watu wengine
2. Kama anajinasibisha anatokea nchi ya nje basi awe amesajiriwa kama travel advisor wa nchi husika (Kuna baadhi ya nchi kama Canada wakijua unafanyiwa maombi na hawa makanjanja hiyo inakuwa sababu ya kukosa) so akuonyeshe uthibitisho kuwa kasajiliwa
3. Amini hisia zako: ukiona konakona au janjajanja mapema tu jitoe
4. Kama anakufanyia mpango invitation letter au mualiko wa mkutano wa kimataifa na wewe jiridhishe mara atakapokutumia
5. Usikubali kufokewa na mtu ambaye umemlipa hela yako. Ukiona mtu anakufokea na hayupo tayari kukupa maelezo hatua kwa hatua basi achana naye tafuta mwingine
6. Sisitiza uwepo wa mikataba wa kazi kama kuna makubaliano yoyote iwe kuirudisha baadhi ya gharama kama utakosa visa basi fanyeni hivyo kwa mikataba wa maandishi ili siku vitu viwe wazi;
NB* : Tahadhari yangu imekuwa inspired na nilivyo- deal na Elly David wa Canada
Sitamani hali hiyo imkute mtu mwingine.
Tunapotafuta safari wakati mwingine tunakuwa tayari kutumia pesa nyingi hata kuvunja vibubu so ni muhimu hiyo pesa ufanye kazi na mtu mwenye uweledi wa hali ya juu na mwenye kuheshimu hela mteja wake!