MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Ninaandika nikiwa na masikitiko makubwa kuona maumbile ya wanawake yanatumika kwenye mambo ya kijinga. Miaka ya hivi karibuni tasnia ya uchekeshaji (comedy) imezidi kuchanja mbuga na kufanya makubwa. Kwa sasa wachekeshaji nao wanaingiza pesa nyingi kama wasanii wengine tofauti na zamani. Wachekeshaji wote walioweza kwenda sawa na uwepo wa mitandao ya kijamii wameweza kuvuna pesa nyingi kutokana na vipaji vyao. Mitandaoni vijana wanapambana ku-upload contents zitakazovuta umati kutazama. Jinsi umati unavyovutika ndo jinsi pesa zinavyoingia. Hakuna longolongo.
Wakati tasnia inavyozidi kukua ndo limejitokeza tatizo la dada zetu waliojaliwa unene na makalio makubwa kutumia maumbile yao katika kuchekesha. Hii ni mbinu ya hovyo na iliyofeli mno. Contents nyingi huwa hazichekeshi zaidi ya kuchochea ngono. Wachekeshaji wengi wenye tatizo hilo ni kutoka Nigeria na hapa Tanzania. Sintotaja majina ya hao wasanii ila mitandaoni wanajulikana. Video nyingi zilizopo ni za kujidhalilisha tu. Hazina mafunzo yoyote wala maadili.
Utashangaa wakati sisi tunakerwa na aina hii ya uchekeshaji kwa wazee wa CHAPUTA kwao ni Full Burudani 😄😄. Yaani hii mijimama inayojifanya comedians imekuwa msaada mkubwa kwa CHAPUTA. Ninawasihi wasanii wetu wajiepushe na aina yoyote ya uchekeshaji ambao hauna maadili.