Kuwa mtu mzima VS Maamuzi

Kuwa mtu mzima VS Maamuzi

Sheffer95

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2020
Posts
211
Reaction score
515
Kama kichwa kinachojieleza hapo, hivi ni kwanini wazazi wetu hasa wa kiume (namaanisha wakina baba) kadri wanavyokuwa wakubwa wanakuwa kama hawashauriki, hasa pale wanapopewa mawazo na watoto wao ambao wamekuwa wakubwa na wanaoa uhalisia wa maisha na changamoto.

Wengi wao huhisi watoto wanapowashauri wanachukua ile power yao waliokuwa nayo kwenye familia, hasa ile ya kusikilizwa na kutekelezewa kila wanalosema.

Je, huu ni mtizamo wangu tu au kuna mtu alishawahi kutana na hali hii. Wababa wengine wanaweza kuwa radhi ku-sabotage hata familia zao ili tu kufuata mawazo yao.
 
Wewe Ni Kaka mkuu? Kama jibu ni ndio subiri kidogo tu, nawe utakuwa baba alafu utaona inavyouma kuona unadharaulika kwenye familia ambayo umeipigania kwa damu na jasho.

Ila ni saikolojia tu. Sio makosa yao, ni ubinadamu tu huo.
 
Wewe ni kaka mkuu? Kama jibu ni ndio subiri kidogo tu, nawe utakuwa baba alafu utaona inavyouma kuona unadharaulika kwenye familia ambayo umeipigania kwa damu na jasho.

Ila Ni saikolojia tu. Sio makosa yao, ni ubinadamu tu huo.
Mm pia ni kaka, Sema inauma sana mzazi anapotaka kuharibu hata Familia sio kwamba Kuna dharau hapana ila Kuna ile namna unaona kama husikilizwi tena. Mbona Akina mama wengi huwa na hekima au wakimya wanapo kuwa wazee kuliko wakina baba?
 
Hiyo tabia wanaongoza wanaume Kanda ya ziwa!..
Nadhani Wababa wengi hupitia hali hii watoto wao wakiwa wakubwa na Hasa wakitaka kushiriki kwenye maamuzi ya Familia
Kiukweli sio kwamba wanaume wanapenda hali hii Sema uhalisia ni kwamba huwa wa nahisi ile thamani Yao kwenye Familia inapotea
 
Sasa kama akili yako haijakomaa atakusikiliza nani. Tafuta pesa uone familia mzima kuanzia baba,mama,wadogo zako mpaka ukoo mzima utakavyokusikiliza. Utaitwa mzee wakati una 25yrs.
 
Sasa kama akili yako haijakomaa atakusikiliza nani. Tafuta pesa uone familia mzima kuanzia baba,mama,wadogo zako mpaka ukoo mzima utakavyokusikiliza. Utaitwa mzee wakati una 25yrs.
😂😂😂😂😂😂
Sawa nashukuru pia kwa maoni yako.
Ila lengo hapa nikuona mwa namna gani hata wanaume tukiwa wazee tuweze jiamini na kutambua nafasi yetu kwenye Familia maana hili lime kuwa tatizo kwenye Familia nyingi
 
😂😂😂😂😂😂
Sawa nashukuru pia kwa maoni yako.
Ila lengo hapa nikuona mwa namna gani hata wanaume tukiwa wazee tuweze jiamini na kutambua nafasi yetu kwenye Familia maana hili lime kuwa tatizo kwenye Familia nyingi

Kuwa na pesa tu hizo heshima na kusikilizwa utakukimbia,hata ukiongea Pumba watu watakupigia makofi wakiwemo wazazi wako.
 
Tafuta pesa kwanza mkuu, utaona vile mnaongea lugha moja na mzee, bila hivyo mzee huwezi ukamwambia kitu akakuelewa.
 
Pima ushauri wa mwanao ukiona una mashiko fanyia kazi . kiukweli haipunguzi kitu kupokea ushauri toka kwa watoto
 
Kuwa na pesa tu hizo heshima na kusikilizwa utakukimbia,hata ukiongea Pumba watu watakupigia makofi wakiwemo wazazi wako.
Ishu sio pesa hapa,
Maana vijana wenye hela ndio wanasikilizwa swali je Akina baba wanajisikiaje au kama wewe ndio baba utajisikiaje maana ulizoea wewe ndio ulikuwa unatoa maamuzi kwenye Familia?!
 
Swala hapa, mfano kijana Ana hela na kwenye vikao vya Familia mawazo yake ya nasikilizwa zaidi na ndugu wanakuja upande wake, je kama baba ambae ndio Mkuu wa Familia aliyekuwa anatoa maamuzi anajisikiaje maana wengi huwa wa nahisi thamani zao zimepotea hivyo wanaenda against ili tu kuonesha wao ndio kichwa cha Familia. Ungekua wewe ndio baba mzazi ungejisikiaje
 
Back
Top Bottom