Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kuna jambo la kushangaza ambalo limeshamiri sana kuanzia mwaka 2016, nalo ni mabango ya picha ya Rais kila mahali. Tabia hii haikuwahi kuonekana wakati wa utawala wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa wala Kikwete.
Najiuliza sana, kama Taifa tunanufaika nini na uwepo wa picha za Rais kila sehemu? Haya mabango ya picha ya Rais yanagharimu kiasi gani cha pesa za wananchi? Hawa wananchi walipa kpdi wananufaikaje na haya mabango? Au kuna wafisadi huko Serikali yanaiba pesa za wananchi kupitia haya mabango? Kama mabango yana faida kwa Taifa, mbona hatuoni hayo mambo kwenye mataifa yote yaliyoendelea? Au tumemfanya Rais ni biashara, hivyo atangazwe kama inavyotangazwa soda ya coca cola? Hivi kuna mtanzania asiyemjua Rais Samia, hadi atangazwe kwa kiwango hicho?
Kwa nini Waafrika tunafanya mambo kama wendawazimu? Kwa nini mambo ya muhimu tunayapa nafasi ndogo sana, lakini yale ya kipuuzi tunayapa umuhimu mkubwa kiasi cha kuchezea pesa ya umma?
Nchi ipo kwenye msiba mkubwa maana waliotakiwa kuwa na hekima zaidi, wamenyimwa hata ile hekima ndogo kabisa, na hivyo kutapanya hata kidogo kinachopatikana. Kuna wakati ilisikika kauli kuwa wananchi hawalipi kodi, kama jweli wananchi hawalipi kodi, hii pesa ya kuchezea namna hii inatoka wapi?