chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,834
- 26,217
Napenda kuisihi Wizara ya Habari kusimamia suala la wakalimani wa lugha ya alama iwe suala la lazima katika vituo vya Televisheni ili kuwapa haki ya kutopitwa na taarifa ndugu zetu wenye changamoto ya usikivu.
Vituo vingi hapa nchini havitoi hiyo huduma na hii ni kutowatendea haki ya msingi ndugu zetu hawa wa makundi maalum.
Aidha nivipongeze vituo vinavyotoa hii huduma ikiwemo Azam Tv na Clouds TV.
Ni wakati sasa umefika vituo vingine navyo viige kwa hiyari au walazimishwe kuajiri wakalimani wa lugha ya alama inapobidi.
Na tunapoelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu na Ule mkuu 2025 basi napo pia tuwe na wakalimani, bila kusahau mikusanyiko yote ile inayotambulika kisheria na kwenye nyumba za Ibada pia.