Kuwa na namba ya simu iliyozoeleka ni mtihani kwa maisha haya

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Teknolojia ni nzuri na kwa mawasiliano haya ya simu, yamesaidia sana watu kuwa kama kijiji kimoja au familia moja.

Ila swala la simu ila kimtazamo naona ni sawa na kufunga pingu pale unapo kuwa na namba ambayo umekaa nayo mda mrefu kwenye maisha yako.

Namba hiyo unakuta ndio unatumia kipindi cha ma Ex,wafanyabiashara mbalimbali,madili,wabaya wako,mliogombana,ulivokuwa ..n.k

Sasa leo nashangaa kuona namba ya Ex wangu bado anayo na mimi sipo naye miaka 12 sasa.

Natamani kutafuta namba nyengine na wakati hii namba ndio kila kitu
 
Huwezi kuwa na EX wa miaka 12 halafu unatumia lugha hiyo ya ....nyengine....hiko kitu.....kimenuka.......kakiwasha......

Wa hizi lugha hawana hata uwezo wa kununua mkanda wa suruali zao.
 
Hiyo ni kawaida ya wanawake sijui huwa wana save wapi namba anaweza akakaa hata miaka mitano akivurugwa kwenye ndoa anarudi mwenyewe kuelezea visa vya mumewe wakati huo walituacha kwa dharau.

N B; ex harudiwi utakuja kuumia zaidi ya mwanzo ukimruhusu awe karibu na ww tena.
 
Sidhani kama anataka kubadili sababu ya kumuogopa Ex….
Imagine Ex atume msg ‘ I miss you darling Kichwa Kichafu, afu mkeo aione. Hapo utajua
Huo sasa ni udhaifu mwingine kama atakua anabadili kumuogopa mkewe.
 
We unaongelea namba,watu wanatunza hadi picha....

Kuna Dada anakujaga ofisini namuhudumuia, kuna siku akaniambia

yani we kaka umefanana na X wangu mpaka basi'', nikamwabia Hebu

nionyeshe huyo X wako nimuone, nikamuona anapekua gallery mara

paap nikaonyeshwa mtu niliefanana nae, Story zikaendelea kama kawaida

mimi nikamuuliza,X wako tangu uachane nae una muda gani hamjawasiliana

ana sema ni miaka,maana ashaingia ktk mahusiano na mtu mwingine,sasa nikawa

nawaza huyu dada mtu wameachana wana miaka anatunza picha yake kwenye simu yanini?
 
Nadhani ni kwasababu ya hisia, wanawake wanaongozwa zaidi na hisia.
 
Sidhani kama anataka kubadili sababu ya kumuogopa Ex….
Imagine Ex atume msg ‘ I miss you darling Kichwa Kichafu, afu mkeo aione. Hapo utajua
Mbona Kuna Njia Nyingi Za Kuepusha Na Kushughulika Na Ex Wapumbafu Kama Hao.

Suala La Kubadilisha Namba Si Kama Umemkwepa Mtu Wa Aina Hiyo.
 
Je ni kweli umefanana na X wake?
Kama ni kweli mmefafa anza kujiongeza dada wa watu tayari ameshamaliza part yake.
 
Ila JF raha sana hata kama una stress pitia tu uta enjoy
 
Me leo nimewaza niwe na namba iliyosajiliwa kwa jina la mtu mwingine. Maana mmh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…