john achila mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 142
- 281
Kuwa na Nywele Fupi au Ndefu Kwenye Ibada kwa Jinsia Zote Mbili
Kumekuwepo dhana mbalimbali kuhusu hali ya nywele, wakati wa ibada. Majibu ya dhana hizo yanapatikana kwenye maandiko.
JINSIA YA KIUME
Kuhusu jinsia ya kiume, Biblia inasema mwanaume hapaswi kuwa na nywele ndefu kwa sababu kichwa chake yeye ni Utukufu wa Mungu.
1Wakorintho 11:3: “Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu. Hivyo kwa mwanaume kuziweka nywele zake kuwa ndefu ni aibu kwake na ni kukiaibisha kichwa chake, ambacho ni Kristo.
14 “Je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake?”
Na siyo tu hatakiwi kuwa na nywele ndefu, bali hata “kufunika kichwa” awapo kwenye ibada, maana yake ni kwamba mwanamume anapokuwa kwenye ibada, hapaswi kuvaa kofia, au kuweka kitu cho chote kichwani kinachoashiria kufunikwa kwa kichwa chake (maana yake kichwa chake siku zote kinapaswa kiwe wazi).
Vile vile, mwanaume hapaswi kusuka nywele, wala kuweka mitindo mitindo kichwani kwa sababu kichwa chake ni utukufu wa Mungu.
Baadhi ya watumishi wa Mungu, hususan Makuhani, hawatakiwi kujifanyia upaa kichwani.
Walawi 21:5 “Wasijifanyie upaa kichwani, wala wasinyoe pembe za ndevu zao, wala wasichanje chale katika miili yao”.
JINSIA YA KIKE
Kuhusu jinsia ya kike, tumesoma kuwa ni aibu kwa mwanaume kufunika kichwa, lakini tukirudi katika jinsia ya kike ni kinyume chake. Kwamba ni aibu mwanamke kuwa na nywele fupi na ni fahari mwanamke kuwa na nywele ndefu.
1Wakorintho 11:15: “Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake. Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya mavazi”.
Kulingana na biblia, wanawake wote ni sharti waache nywele zao ziwe ndefu. Kuzikata nywele au kuzifanya fupi, pasipo sababu yo yote ya msingi kama vile magonjwa, au udhaifu wa mwili, ni kwenda kinyume na maagizo ya Mungu.
Ndiyo maana upara huwa hauwapati wanawake, bali wanaume tu. Hiyo siyo kwa bahati mbaya, la hasha. Hiyo ni kuonyesha kuwa wanawake wamekusudiwa kuwa na nywele vichwani mwao wakati wote wa maisha yao, na wanaume ni kinyume chake.
Na zaidi, biblia inazidi kuelekeza kuwa hata kama mwanamke atakata nywele zake kutokana na matatizo fulani, labda magonjwa au kutokana udhaifu wa nywele kukatika zenyewe, basi hapaswi kutembea nje akiwa na nywele zake hizo fupi, bali anapaswa afunike kichwa chake kwa kitambaa au kwa kitu chochote kile.
1Wakorintho 11:6 “Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.
7 Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume”.
Mwanamke anapokuwa kwenye ibada, awe na nywele ndefu au fupi, ni Agizo la Bwana, kwamba afunike kichwa chake.
Kuna sababu kuu mbili:
Kwanza: ili asikiabishe kichwa chake ambacho ni mwanaume.
Pili: kwa ajili ya malaika.
Tunapokuwa kwenye ibada, malaika wa Bwana wanahudumu pamoja na watakatifu. Malaika hawa Bwana aliowaweka kwa ajili yetu wana uhusiano mkubwa sana sisi katika kutuhudumia (Mathayo 18:10).
Kwa hiyo, tunapokuwa kwenye ibada na ndani yake kukawa kunafanyika mambo ambayo ni kinyume na Neno la Mungu, malaika hawa wanaondoka, na hivyo kufanya ibada kupoa na utukufu wa Mungu kupungua.
Pia, wanawake hawapaswi kusuka nywele zao, au kuvaa wigi, au kuzibadilisha maumbile nywele zao, aidha kwa kuziweka kemikali, au dawa za kuzifanya zilale.
Kuhusu kuvaa wigi, kunachukuliwa kuwa ni ibada ya miungu au ibada ya sanamu (Kutoka 23:32; Warumi 12:1-2; 1Wakorintho 10:14, 19-22). Hivyo, hairuhusiwi, hata kama zinavaliwa na baadhi ya wakristo.
Biblia haijawapa maagizo ya kuzifanya nywele zilale au zing’ae au ziwe kama za jamii ya watu fulani, bali mesema, “ziwe ndefu”, basi.
1Timotheo 2:9 “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna”.
Kwa ujumla, kulingana na maandiko, kichwa cha Kristo ni Mungu (1Wakorintho 11:3).
Kuhusu mwanaume, maandiko hayo yanamtaka awe na nywele fupi, kwani kichwa cha kila mwanamume ni Kristo.
Kwa upande mwingine, maandiko yanamtaka mwanamke awe na nywele ndefu, kwa sababu kichwa cha mwanamke ni mwanamume. Pale ambapo kuna changamoto yo yote kuhusu kichwa au nywele, basi afunike kichwa chake.
Pamoja na hayo, maandiko yamekataza uvaaji wa nywele bandia (wigi) kwa jinsia zote mbili, kwani ni sawa na ibada ya miungu/sanamu (Kutoka 23:32; Warumi 12:1-2; 1Wakorintho 10:14, 19-22).
Pamoja na kwamba kwenda kwenye ibada, ni uamuzi binafsi kwa wanaume na wanawake kuwa na nywele ndefu au fupi, au kuvaa wigi, kwa kujua au kutokujua, maandiko, kama ilivyoainishwa kwenye somo hili hapo juu, ndiyo yanatawala ni nini sahihi kifanyike.
Ni heri kufuata maandiko yanavyohitaji ili kukwepa kumchukiza Mungu.