Kuwa na vyeti vingi sio kigezo

Kuwa na vyeti vingi sio kigezo

Huko kwenye interview ulikutana na wenye degree au diploma ya CS?
 
Huo mshahara unaolipwa, soma masomo ya jioni upate chet cha four, au mtafute mwalimu wa masomo akufate kukufundishia nyumbani, mambo yanaweza geuka, mfano watu wangapi wapo nyumbani kwa ajiri ya vyet vya four na walikuwa na Ajira zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba waheshimiwa mnielewe kwenye huu uzi nilioandika hapa...

Kumekua na tabia ya watu waliosoma degree au masters au level zingine za elimu ya juu kuwakatisha tamaa wale ambao hawaja fanikisha kupata elimu hizo.

Leo nataka tuwekane sawa ili kama ulikatishwa tamaa na kuhis huwez kupata ajira sabab tu hujafanikiwa kupata hayo mavyeti bas leo upate nguvu upya, natumia mfano hai wa KWANGU mwenyewe. Sikufanikiwa kuhitimu form4 niliishia form3 kwa sabab za kiuchumi ila darsan nilikua smart (nilikua na faulu masomo vizur) baada ya shule kuishia njian nilipata vibarua kwenye site za ujenz nikabeba zege kwa hasira nikafanikiwa kutunza hela ambayo nililipa fee ili kusoma coz ya CISCO(hii niliisoma online ikiwemo ku google, youtube zote zilihusika) nikafanya exam nikafaulu na kua certfied CCNA then nika cheza mchezo nikapokea bada ya miez mi4 hiv nikalipa tena fee nikasoma CISCO tena level inayofuata ambayo ni CCNP, nikafanya exam nikapata certificate. Nikafanya na coz ya ITIL Foundation.

Ikumbukwe ada za kufanya hayo yote ni ile kaz ya site ya zege nilikua nalipwa 7,000/day. Halaf nikawa nacheza mchezo so nikipokea hela ya mchezo ndo nalipa fee. Baada ya kua na CCNP na ITIL Foundation nikaanza kutafuta sehem za ku volunteer Mungu ni mwema nikapata nikaanza kufanya kama IT TECHNICIAN ndan ya miez 6 maisha yalikua magum lakin nilkomaa coz natafuta uzoefu wa kazi.

Mungu akazid kua mwema nikaajiriwa pale pale na position ika change nikawa SYSTEMS ADMINISTRATOR. Na walijua sikua na chet cha form 4. Nikfanya kwa miaka 3 nikaona post mtandaon anahitajika NETWORK ADMINISTRATOR sikulemba nikatupa CV yangu hyo hyo isiyo na chet cha form4 ila uwezo wangu wa kufanya kazi ulikua mkubwa. Nikaitwa interview nikapitia tulikua 15 ambapo wenzangu wote walikua wana diploma za IT na computer science lakin walifel practical hapo ndo mm nisiokua na vyeti nikachomoa betri yaan niliwapita kama rocket hadi IT MANGER akaniulizaat umeaema hukumaliza form 4 au umesema hukumaliza chuo!!

Na hapa ndo nilipo hadi sasa napokea watu wa field kutoka vyuo maarufu kama DIT NA DSM na mm ndo Eng. Wao hapa upande wa vitendo. Wao wanakuja na theory ambazo tunaziweka pemben mim nawapa kanun za kufanya kazi.

Hitimisho: haijalish una elimu kias gan kila kitu kinawezekana songambele usikate tamaa na maneno ya wanye degree wakikwambia et wasomi ni wengi we hata form 4 hujamaliza utaajiriwa na nan. Hao ni wanga. Naishkuru google kuniwezesha kusoma online huku nikwa nabeba zege ili kupata fee.

Huo ni uongo...eti hata form four hujamaliza na acha kupotosha umma


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sasa we jamaa unasema huna vyeti au huna cheti cha form foo? Si umesema ulisoma ma Cisco hayo ukamaliza au? Hizo kozi za foundation ulipomaliza hawakukupa cheti? Navyofahamu Mimi ukisoma hata kama ni mtandaoni ukimaliza wanakupa cheti. So wewe Una vyeti vya IT kazi unayofanya Ila huna cha form foo. Usiwadanganye watoto wa watu wakaacha kumaliza secondary.

Nadhani mantiki ya Uzi wako ingekuwa mtu unaweza kupata kozi ukasoma na ukamaliza mtandaoni bila kuwa na cheti cha form foo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom