Kuwabana Wakurugenzi kuhusu V8 ni usaliti wa CCM na Serikali yake kwao. Bila wao hali ingekuwaje?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa, Miji na Miji Midogo ndiyo waliopanga na kupangika kwa mipango iliyoiwezesha CCM kushinda kwa kishindo. Wao ndiyo walioratibu taratibu bila tabu mbinu zote za ushindi wa CCM kwa mwamvuli wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Wakurugenzi ndiyo walipokea maagizo ya kufanikisha ushindi 'kwa vyovyote vile'. Wakatekeleza. Ushindi ukapatikana.

Kitendo cha kuwabana, kuwasema, kuwasimanga na kuwaumbua Wakurugenzi kwa ununuzi tu wa magari aina ya V8 ni kitendo cha kuwasaliti kichama na kiserikali. Ni kitendo cha kutowalipa vyema fadhila kwa wema walioufanya kwa chama na Serikali wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Sote tunajua, mchakato wa ununuzi wa magari hayo unahusisha ofisi mbalimbali za kiserikali.

Tunajua kuwa ununuzi ulifuata taratibu na kupata baraka zote. Kuwafanya Wakurugenzi ni mbuzi wa kafara katika hili la ununuzi wa ma-V8 si sawa wala si jambo la afya. Wakurugenzi wanastahili heshima pamoja na uwezekano wa kutumbuliwa muda wowote aupendao Mteule wao. Wakurugenzi walikibeba chama uchaguzini, nao wabebwe kwenye utumishi wao. Waachwe, wenye Halmashauri zenye uwezo, kununua ma-V8 ili nao walie kivulini.

Lengo lilikuwa kuufuta upinzani, imekuwaje sisi wenyewe tena kulazimisha uwepo Bungeni?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)
 
Wakurugenzi hawakua na sababu ya kununua magari ya gharama kiasi hicho.
Wameonyesha wazi kwamba wao hawana vipaumbele wala hawakubaliani na dhana ya kupunguza gharama zisizo za lazima kwa maendeleo ya nchi
 
Liangaliwe pia suala la miundombinu ya barabara huko wanakuhudumu. Majukumu ya kazi yakiwahitaji kutembelea pembe mbalimbali za wilaya. Mayunga mkono hoja
"Don't bit the hands that feed you" mabeberu hunena wakurugenzi ndio mastermind wa ushindi wa kishindo lazima walipwe fadhila
 
Wakurugenzi hawakua na sababu ya kununua magari ya gharama kiasi hicho.
Wameonyesha wazi kwamba wao hawana vipaumbele wala hawakubaliani na dhana ya kupunguza gharama zisizo za lazima kwa maendeleo ya nchi
Hao woote ni makada wa ccm
 
Hoja yako ni ya Msingi sana na ina mashiko...

Naunga hoja mkono....
 
Wakurugenzi hawakua na sababu ya kununua magari ya gharama kiasi hicho.
Wameonyesha wazi kwamba wao hawana vipaumbele wala hawakubaliani na dhana ya kupunguza gharama zisizo za lazima kwa maendeleo ya nchi
Vipi malipo ya wabunge, kila mwezi na wanapomaliza miaka mitano?
 
VUTA-NKUVUTE umenena vyema. Wewe una busara kubwa. Nyongeza kwenye hoja zako ambazo naziunga mkono. Waswahili wana misemo yao kuhusu kumtendea mtu au mfumo fadhila na mrejesho kutoka kwa mnufaika.
Pia hao wakurugenzi wanasafiri sana bila kuwa na magari yenye hali ya utulivu wengi wataishia kuugua vifua, matatizo ya migongo ya kudumu na kufa vifo vya mapema. Pia ufanisi wao kazini utahadhiriwa na mazingira magumu ya kazi ikiwemo magari yasiyoendana na na kazi ngumu zenye mashinikizo wazifanyazo. Jamani Watanzania tuwatendee vema binadamu wenzetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…