Kuwaburuza wabunge wanaojitambua ni kuburuza wananchi, sasa Dkt. Tulia naye tumpeleke kwa wananchi ashughulikiwe

Na siamini hata kwa sekunde moja, kwamba yanayofanywa na Bashe ni yake mwenyewe. Hana uwezo na hata ujasiri wa kuyafanya hayo.
Nakuunga mkono kwenye kabisa! Haya mambo ya hovyo yafanywayo na viongozi ni maagizo ya chama chao CCM na ndio maana huoni wakiwa waoga wala wenye aibu watendapo.
Pia ona nguvu itumikayo kuwalinda! Hicho kispika kinakomaa kama kichawi kukazia maumivu.
 
Mkuu unakumbuka kanuni zilizotumika kuwasulubu wapinzani kipindi cha Ndugai???

Walidhani kanuni zile ni mahususi kwa ajili ya wapinzani, sasa ndio zinatumika kwao.

Ndio maana uliona wabunge wote kimyaaaa, hata Olesendeka ulimuona na kiherehere chake??

Mkuu maji ya kinyozi yapo tayari!!

Sheria ni msumeno, na Mpina akitoka nje anashughulikiwa pia in Magufuli's words!!

⚖️4Asimwe#
 
Watachagua mwingine ambae atakuwa upande wa serikali. Atakuwa puppet again. The best way ni katiba ibadilishwe of how speaker anapatikana else tunazunguka pale pale

⚖️4Asimwe#
 
Safi, kama mabadiliko ya katiba yatawalinda wabunge wetu wanaosimamia maslahi ya wananchi basi ni jambo jema kabisa. Kwetu sisi wananchi mbunge bora ni yule anayeiwajibisha serikali kwa niaba yetu bila kujali ni wa chama gani.


⚖️4Asimwe#
 
Wananchi gani mkuu. Hawa hawa ambao wao wakishapewa kofia na zuchu kuwakatia mauno stejini wanatoa mitano tena. Hawa hawa ambao wanaamini viongozi kupiga ni haki yao na wao kila wanachofanyiwa ni hisani na inabidi washukuru sana?
Kufikia sasa hivi ingekuwa nchi inayojielewa na vyombo vyenye uhuru ilibidi TAKUKURU wawe kazini kuchimbua mzizi na ukweli wa haya yote maana Bw. Mpina kawapa direction na ushahidi lakini TAKUKURU ni taasisi ambayo huwa mpaka iagizwe kufanya kazi na wale ambao inabidi iwachunguze. Huwa sioni hata sababu ya uwepo wake maana haifanyi kazi yake zaidi ya kudeal na watu wa chini kabisa.
 
Huyo speaker kwa jinsi alivyotaka kupitisha ule mkataba na dubai kwa hila bungeni na pale alipowaita wote wanaoupinga wapumbavu sina imani naye kabisa. Namuona kama mamluki wa ubeberu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…