Wakuu, juzi katika vikao vyetu vya pombe tulikumbana na hoja moja iliyokuwa moto sana hasa kwa akina mamsapu!!!
Hoja yenyewe inahusu kupima DNA watoto wetu wanapozaliwa; mimi nilitetea kwa hoja kwamba inasaidia watu kuwa makini wanapomega au kumegwa nje, na pia inaleta faida kwa mtoto kwa kumjua baba halisi
Pia nilitetea hoja kwamba hakuja ubaya kutumia utaalam wa kisayansi uliopo kwenye maisha ya kila siku
Cha kushngaza, wanawake woote waliokuwa pale (including tibaigana wangu) walipinga DNA tena kwa hasira kabisa na hasa wakisisitizia kwamba kupima DNA ni kumfanya mkeo kuwa si muaminifu
sasa wadau, naombeni mawazo yenu kwani bado naamimi DNA ni ,uhimu!! akina dada mnasemaje?