Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Nawasalimu Kwa jina la Jamhuri;(Itikieni: Kazi iendelee).
Wizi sio mzuri lakini kuna Watu watanicheka na kusema huyu anaongea nini. Anyway! Inategemea na Aina ya wizi, hapo vipi? Lakini Mimi ninajua wizi ni wizi tuu! Mmmh! Hapana wizi hauwezi kuwa wizi tuu! Upo wizi mzuri na upo wizi Mbaya.
Kivipi?
Sikiliza Bwana Mdogo, kitu chochote chenye matokeo mabaya huwa ni kibaya, na kitu chochote chenye matokeo mazuri ni kizuri." Unamaanisha upo wizi wenye matokeo mazuri?
"Upo wizi wa kuibia wajinga, vipofu na wanyonge ambao hawajui wanaibiwa, wizi huo ni mzuri Kwa sababu hauna madhara"
Mimi sitaki mafundisho yako bhana, ninachojua Wizi ni wizi tuu! Hakuna wizi Mzuri, wizi ni Mbaya.
"Tatizo lako Taikon unajifanya Mjuaji lakini huna unachojua, sikiliza, wizi Mbaya ni ule wa wajinga, vipofu na wanyonge kuibiana. Huo wizi unamadhara kwao wenyewe Kwa sababu watauana au kupelekena jela na kufungana korokoroni.
Unajua Taikon wewe bado ni kijana mdogo, bado ni mchanga Sana kuna mambo huyajui, mjinga hawezi kujua anaibiwa na mwerevu, mjinga anaweza kujua anaibiwa na mjinga mwenzake, kipofu hawezi kuona anaibiwa na mwenye Macho yenye kuona, Ila atajua anaibiwa na kipofu mwenzake, hivyohivyo na Mnyonge hawezi kujua anaibiwa na Tajiri Ila atajua akiibiwa na mnyonge mwenzake"
Huwezi Kupata madhara ukiibia wajinga, vipofu na wanyonge. Hiyo Ipo hivyo. Pengine haihesabiki kuwa ni Wizi.
Nataka kukuambia Taikon, Mjinga anamheshimu mtu anayemuibia Kwa sababu hajui anaibiwa. Kumuibia mjinga na kipofu ni rahisi Sana na inafurahisha Kwa sababu unamuibia alafu anakuona umebarikiwa na Mungu, anaona Mungu ndiye aliyekustawisha na kukujalia Maisha mazuri. Asijue wizi wako ndio umekunufaisha.
Ni rahisi kuwaibia Wajinga Kwa sababu zifuatazo:
1. Hawajui wanaibiwa.
2. Hawana umoja
Moja ya zile Sifa kuu za Watu wajinga Ni kukosa umoja. Hawawezi kuwa na umoja Kwa sababu wao ni wajinga, hawajui umuhimu wa umoja. Hahaha! Kwa hiyo wewe ukija ni kupiga tu. Wajinga Ni kama Preys ambao huwindwa na Predators. Wajinga Ni kama Kuku kwenye Banda wanaofugwa, ukiamua muda wowote unakamata unachinja unakula zako. Hawawezi kuungana kupingana na matatizo Yao. Hiyo ni tofauti na watu Werevu, wao ni Wamoja, watapambana kwa mbinu zozote ziwe za Amani au za hatari ili kulinda umoja wao kwani umoja wao ndio nguvu Yao.
3. Wanaamini katika majaliwa
Wajinga Ni Watu wasiowajibika, wanaamini Maisha Yao yanaamuliwa na mhusika mwingine iwe anayeonekana au asiyeonekana. Maisha mazuri kwao ni kama hisani. Mimi bado sijakuelewa, maelezo mengi lakini hayaeleweki. "Hakuna asiyekujua Taikon, wewe ni mbishi kama wale Watu wa kule ziwa Tanganyika, kama hujaelewa shauri yako. Nenda jela ukaone ni kina Nani wamefungwa Kwa kesi za wizi ili uelewe nikisemacho"
Mimi siwezi kuelewa chochote hapo. Wizi ni wizi. Hakuna wizi Mzuri. Come on!
ATI wadau huyu Mzee mnamuelewa? Mnakubaliana naye kuwa kuna wizi Mzuri na wizi Mbaya?
Nawatakia jumapili Njema!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi.
Kwa sasa Dar es salaam