Kuwakamata na kuwaweka mahabusu kunanachangiaje maendeleo ya Tanzania?

Kuwakamata na kuwaweka mahabusu kunanachangiaje maendeleo ya Tanzania?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Hii kamata kamata ya viongozi wa upinzani nchini inasaidiaje kuondoa umaskini? Je wanapopelekwa mahabusu wanatumika katika kufanya uzalishaji au wanakaa tu wakisubiri wapate dhamana au wahukumiwe? Lakini pia hii ipo kwenye ilani ya chama Cha mapinduzi au imeandikwa wapi kwamba ni.marufuku wapinzani kufanya siasa Tanzania?

Let assume huyo mtoa amri nafsi yake inafarijika akisikia katika utawala wake amekamata wapinzani wote na kuwatia ndani, je hii furaha yake inasaidiaje kutengeneza mshikamano na umoja wa Taifa? Tunakubaliana unaweza ukazaliwa na roho mbaya na kwamba hakuna namna roho yako mbaya itaondoka ukipewa madaraka makubwa kwa sababu wakukukanya watakuwa wachache au wasiwepo,ila unanufaikaje na hiyo roho ya kikatili? Mshahara wako unaongezeka? Miaka ya kuishi inaongezeka?

Wananufaikaje wanaotenda haya? Haiwekani kuongoza bila kunyanyasa wale unaowaongoza na familia zao? I'm confused, nini mtawala wa kiqfrika upata pale anapotumia madaraka kukandamiza familia za wasio na madaraka?
 
Ni MATUMIZI mabaya ya Madaraka yaliyojaa UONEVU VISA VISASI MATESO ROHO MBAYA CHUKI ya wenye Madaraka
 
Kijana haujui nini maana ya amani. Burundi, Congo, Centre Africa, Sudan, Msumbiji na kwengineko walianza hivi hivi vimaandamano uchwara, uwanaharakati wa hovyo nk matokeo yake leo hii nchi hizo zipo katika machafuko makubwa ambayo yameharibu uchumi wa nchi zao.

Serikali haiwezi kuona viashiria vya uvunjifu wa amani kupitia wajinga wachache afu ikae kimya kusubiri matokeo. Waswahili wanasema "mdharau mwiba mguu huo tende". Pia "ukimchekea nyani shambani utavuna mabua".
 
Haki haiombwi haki hudaiwa

Hatuhitaji kutia huruma ila tupate haki yetu

Hakuna wa kukuhurumia hapa

Pambania haki yako kwa namna yoyote inayowezekana wenzetu wenye udhubutu wanaumia huko mahabusu

Hakuna umoja

Kama wote tusiopenda haya yanayoendelea nchi hii tungetoka kuunga mkono mapambano yanayoanzishwa na hawa viongozi wetu tungefaulu mapema tu na hakuna ambaye angekuwa yuko ndani

Lakini keyboard

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom