Kuwalinganisha wasemaji Masau Bwire na Thobias Kifaru si kumtendea haki Kifaru

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,421
Reaction score
1,395
Kuwalinganisha wasemaji wa klabu Masau Bwire wa Ruvu Shooting na Thobias Kifaru wa Mtibwa Sugar kwamba wana tabia zinazofanana si kumtendea haki Kifaru. Huyu jamaa wa Mtibwa mara nyingi nimemsikia akiukubali muziki wa timu pinzani wanapofungwa na akieleza mapungufu ya timu yao huku mara zote akimnukuu kocha wao. Hazungumzii mechi zinazofuata kwamba lazima watashinda bali husema kocha anawaandaa vijana vizuri kuikabili mechi hiyo. Hawalalamikii sana waamuzi timu yake inapolala.
Bwire siku zote anakuwa mtu wa majisifu tu kwa timu yake. Huongelea mechi zinazofuata kwa kutamba kwamba lazima timu yao itashinda. Timu yake ikipoteza mchezo mara nyingi hulaumu waamuzi lakini ikishinda hana neno baya kwa waamuzi na mara kadhaa huwapongeza. Sasa anasema baada ya kumfukuzisha kocha wa Ndanda, makocha wengine wa timu watakazokutana nazo wajiandae kufukuzwa! Hii si lugha ya kiuana michezo kabisa ya kuongelewa na kiongozi wa timu, ya kushangilia masahibu yaliyomkuta mdau mwenzako wa michezo.Maafisa Habari wa klabu msijisahau kwamba nyinyi ni viongozi wa klabu na si mashabiki wa timu. Mnapaswa muongee ki-uongoziongozi na si kishabikishabiki

Thobias Kifaru: Kiongera, Kwizera ni wauza mitumba

Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru, amesema kuwa Simba haijafanya usajili wowote wa maana na ndiyo maana inaogopa kucheza mechi ya kirafiki dhidi yao.
Kauli hiyo imekuja ikiwa ni baada ya Simba kukataa kucheza na Mtibwa katika mchezo maalum wa kufanya majaribio ya tiketi za kielektroniki, uliokuwa upigwe leo Ijumaa kwenye Uwanja wa Taifa.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Kifaru alisema Simba waliogopa muziki wao kwa kuwa usajili wao hauna lolote na kudai kuwa wachezaji wao wapya wakiwemo Paul Kiongera na Pierre Kwizera ni sawa na wafanyabiashara wa mitumba na siyo wachezaji hatari.
"Mtibwa siyo timu ndogo ndiyo maana Simba wameogopa, hao wachezaji wao wapya ni wauza mitumba. Mimi siamini kama ni wachezaji wa kimataifa. Wanatudanganya tu, wanatuletea watu wa mitaani, wanasema ni wachezaji," alisema kwa kujiamini.
Simba, imepanga kujipima dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya, Gor Mahia, kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini.

Source: Gazeti la Championi Thobias Kifaru: Kiongera, Kwizera ni wauza mitumba - Global Publishers

cc: Revocatus Kashaga
 
Wote ni wale wale tu wanasaka tonge kwa kutumia uwezo wao wa kubwabwaja...
 
Masau Bwire yupo vizuri sana;
Ref: "Mpira wa miguu si sawa na kuuza mayai"
 
Ni wasemaji ambao unatamani kuendelea kuwasikiliza iwapo tu timu yako haijapata kipigo toka kwao.

Naunga mkono hoja kwa 100%. Napenda sana kuwasikiliza timu zao zinapoifunga Simba, lakini huwa sipendi na wala siwasikilizi kabisa pale Yanga inapokutana na kipigo au hata sare tu kutoka kwa timu zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…