Jospina
JF-Expert Member
- Apr 19, 2013
- 2,421
- 1,395
Kuwalinganisha wasemaji wa klabu Masau Bwire wa Ruvu Shooting na Thobias Kifaru wa Mtibwa Sugar kwamba wana tabia zinazofanana si kumtendea haki Kifaru. Huyu jamaa wa Mtibwa mara nyingi nimemsikia akiukubali muziki wa timu pinzani wanapofungwa na akieleza mapungufu ya timu yao huku mara zote akimnukuu kocha wao. Hazungumzii mechi zinazofuata kwamba lazima watashinda bali husema kocha anawaandaa vijana vizuri kuikabili mechi hiyo. Hawalalamikii sana waamuzi timu yake inapolala.
Bwire siku zote anakuwa mtu wa majisifu tu kwa timu yake. Huongelea mechi zinazofuata kwa kutamba kwamba lazima timu yao itashinda. Timu yake ikipoteza mchezo mara nyingi hulaumu waamuzi lakini ikishinda hana neno baya kwa waamuzi na mara kadhaa huwapongeza. Sasa anasema baada ya kumfukuzisha kocha wa Ndanda, makocha wengine wa timu watakazokutana nazo wajiandae kufukuzwa! Hii si lugha ya kiuana michezo kabisa ya kuongelewa na kiongozi wa timu, ya kushangilia masahibu yaliyomkuta mdau mwenzako wa michezo.Maafisa Habari wa klabu msijisahau kwamba nyinyi ni viongozi wa klabu na si mashabiki wa timu. Mnapaswa muongee ki-uongoziongozi na si kishabikishabiki