Kuwaondoa Wamachinga ni bomu linalosubiri kulipuka

Kuwaondoa Wamachinga ni bomu linalosubiri kulipuka

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2021
Posts
3,085
Reaction score
4,890
Hakika nadhani zile kauli za Viongozi kuwa MACHINGA WASIBUGUZIWE waacheni Wafanye Biashara popote na tukawatengenezea Vitambulisho vya kuwatambua na kuchukua Sh.20,000/= sasa Madhara yake ndio Yameanza kuonekana.

Watanzania TUACHE SIASA kwenye kila Kitu. Sasa hivi Machinga hapo Walipo ndipo Wanapopata Mkate wao wa kila Siku wao na Wazazi na Familia zao.

Kuwaondoa kwa HIARI na Kuwapeleka Maeneo Mengine itakuwa ngumu sana na kama Nguvu itatumika basi MADHARA yake ni MAKUBWA sana.

Tujifunze Kuwa na Utaratibu wa KUFUATA Sheria na Mipango sio kila kitu tunaweza Siasa ETI NI WAPIGA KURA WETU
 
Yaani WAFANYE BIASHARA BILA YA UTARATIBU ili "bomu lisilipuke" ?!! Khaaa 😲🤣🤣

Jambo lenye kukosa UTARATIBU NA KANUNI ni KELELE NA BUGDHA.

Nchi haiongozwi KIHISIA.
 
Wakome maana kipindi cha kampeni huwa wanatumika na CCM, baada ya hapo kila mtu apambane na hali yake
Unadhani wamachinga wote ni wajinga kutoielewa serikali na KANUNI WALIZOLETA KWA WANABIASHARA?!!!Khaa 😲😲
 
Halafu aliyeleta sokomoko keshajifia zake,eti wapiga kura! Kwahiyo yeye aliona wanaopiga kura nchi hii ni machinga tu!
 
Wakome maana kipindi cha kampeni huwa wanatumika na CCM, baada ya hapo kila mtu apambane na hali yake
Hizo ni miongoni mwa faida za kudanganywa na kukubali kwa ugali wa siku moja, kama sii zile kofia za bure, t-shirt, madela na vingine vidogo vidogo vyevye rangi mbogamboga.
 
Subiri 2025 ikaribie watarudishwa kwa nguvu kubwa sanaaaa
 
Wamachinga wanasema watainyima kura CCM,wamesahau kuwa tume na katiba yetu Ni ileile na siku chache zilizopita hawakuwa na mpango was kuongelea katiba Mpya Wala tume huru,Sasa sijui hizo kura zao zitasaidia Nini?
 
Madhara yameanza kuonekana hata mwezi ukiwa haujaisha

Pesa haipo mtaani, vijana wapambanaji tunaelewa

Kama umeajiriwa unalipwa mshahara kwa mwezi au Ni uvccm unapata posho ya vikao HII Mada haikuhusu.
 
Kwani kazi ya polisi ni nini? Kwa hiyo wamachinga wawepo Ili wizi uishe, hiyo haikubaliki. Huo ni upepo ambao polisi hawapaswi kuunyamazia..watu wale Shaba za kichwa ndani ya mwezi watu watarudi kijjini kulima
 
Huu mwaka mpaka uishe kutakua na matukio mengi Sana ya uhalifu.

Na sio kwamba wanafanya uhalifu wakastarehe,

Wengine wanafanya uhalifu wakalishe tu familia zao.

HAPA SERIKALI IMECHEMKA
 
Back
Top Bottom