Kuwapenda Adui Zetu Katika Maisha ya Kila Siku

Kuwapenda Adui Zetu Katika Maisha ya Kila Siku

John Magongwe

Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
71
Reaction score
119
Kuwapenda Adui Zetu Katika Maisha ya Kila Siku

Katika mahubiri yake, Yesu alisema, “endeleeni kuwapenda adui zenu” (Mathayo 5:43-44; Luka 6:27, 35). Maneno haya yanamaanisha tunapaswa kuwatendea kwa upendo wale wanaotuchukia au kututendea vibaya. Hakuna mtihani mgumu ambao Kristo alitupa katika sheria ya upendo kama hii ya kumpenda adui yako. Bwana anasema "Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi" (Mathayo 5:44).
Yesu mwenyewe aliwaonesha upendo maadui wake kwa kuwasamehe wale waliomtendea kwa njia isiyofaa. (Luka 23:33-34). Mafundisho yake kuhusu kuwapenda maadui wetu yanapatana na mambo yanayozungumziwa katika maandiko (Kutoka 23:4-5; Methali 24:17; 25:21).

Kwa Nini Uwapende Adui Zako

Mungu mwenyewe ametuwekea mfano
: Mungu “huwaonyesha fadhili hata watu wasio na shukrani na waovu” (Luka 6:35). Yeye “huwaangazia jua lake waovu” (Mathayo 5:45).

Upendo unaweza kumchochea adui kubadilika: Biblia inasema kwamba tumtendee adui kwa fadhili, na inasema tunapofanya hivyo, “tutakuwa tunakusanya makaa ya mawe yanayowaka juu ya kichwa chake” (Methali 25:22). Maneno hayo ya mfano yanarejelea kazi ya kupitisha chuma kwenye moto ili kupata madini. Vivyo hivyo, tukimwonesha fadhili mtu anayetuchukia, huenda tukayeyusha hasira yake na kutokeza sifa zake nzuri.

Utawapendaje Adui Zako

Watendee mema wale wanaokuchukia
(Luka 6:27): Biblia inasema, “Ikiwa adui yako ana njaa, mlishe; ikiwa ana kiu, mpe kitu anywe” (Warumi 12:20). Huenda ukapata njia nyingine za kuonyesha unampenda adui yako kwa kutumia maandiko yanayosema: “Kama vile mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo”(Luka 6:31).

Wabariki wale wanaokulaani (Luka 6: 27-28): Tunawabariki adui zetu kwa kuzungumza nao kwa fadhili na ufikirio, hata wanapotutukana. Biblia inasema kuwa, “Msilipe matukano kwa matukano. Badala yake, lipeni kwa baraka” (1Petro 3:9). Maneno hayo yanaweza kutusaidia kushinda chuki.

Sali kwa ajili ya wale wanaokutukana (Luka 6:28): Mtu anapokutukana, usimlipe “uovu kwa uovu” (Warumi 12:17). Badala yake, muombe Mungu amsamehe mtu huyo (Luka 23:34; Matendo 7:59-60). Badala ya kulipiza kisasi, mwachie Mungu amshughulikie mtu huyo kulingana na kiwango Chake kikamilifu cha haki (Mambo ya Walawi 19:18; Warumi 12:19).

Uwe mwenye subira na fadhili (1Wakorintho 13:4). Katika ufafanuzi wake unaofahamika sana kuhusu upendo, Mtume Paulo alitumia neno la Kigiriki (agape) ambalo tunapata katika maneno ya Mathayo 5:44 na Luka 6:27, 35. Tunaonyesha upendo kama huo wa Kikristo hata kuelekea adui zetu tunapowaonesha subira na fadhili, bila kuwa na wivu, kiburi, au ukaidi.

Upendo ni wenye subira na fadhili: Upendo hauna wivu. Haujigambi, haujivuni, haujiendeshi bila adabu, hautafuti faida zake wenyewe, hauchokozeki. Hauweki hesabu ya ubaya. Haushangilii ukosefu wa uadilifu, bali hushangilia pamoja na kweli. Huhimili mambo yote, huamini mambo yote, hutumaini mambo yote, huvumilia mambo yote. Upendo haushindwi kamwe (1Wakorintho 13:4-8).

Mistari ya Biblia Kuhusu Kuwapenda Adui Zako

Luka 10:29-37
: Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe. Maandiko yanasema "Yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake" na pia "Mtu akisema, nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona"
Luka 23:34: Biblia inaonyesha kwamba unaweza kumpenda mtu bila kukubaliana na mwenendo wake usiofaa. Kwa mfano, Yesu alishutumu jeuri lakini alisali kwa ajili ya wale waliomuua.
Kutoka 23:5: “Ukimwona punda wa mtu anayekuchukia amelemewa na mzigo na kuanguka, usimpuuze na kwenda zako. Unapaswa kumsaidia kufungua mnyama huyo”. Hii inaonesha kuwa tunampenda adui yetu kwa kumsaidia.
Methali 24:17-18: “Adui yako akianguka, usishangilie, na akijikwaa, usiruhusu moyo wako uwe na shangwe; la sivyo, Mungu ataona jambo hilo naye hatafurahi”. Mungu hataki tushangilie, hata kisiri, kuhusu mambo mabaya yanayowapata maadui wetu.
Luka 6:28: “Kuwabariki wale wanaowalaani, na kusali kwa ajili ya wale wanaowatukana.”. Hii ina maana kuwa zungumza kwa fadhili na heshima kuwaelekea wale wanaokuchukia au kukutendea kwa njia isiyo ya haki, na uombe Mungu awasamehe.
1Petro 2:23: Yesu alipokuwa akitukanwa, hakujibu kwa kutukana. Alipokuwa akiteseka, hakutoa vitisho, bali alijikabidhi mkononi mwa Yule anayehukumu kwa uadilifu. Ni kwamba Yesu alimwachia Mungu kazi ya kushughulikia ukosefu wa haki.
1Petro 3:9: “Msilipe ubaya kwa ubaya au matukano kwa matukano”. Hii ina maana kuwa badala ya kulipiza kisasi, jaribu kutatua matatizo kwa amani.

Kujihusisha katika Vita Dhidi ya Adui Zako
Hatupaswi kujihusisha na vita hiyo. Kumbuka kuwa Yesu aliwafundisha wafuasi wake wasipigane kuhusu maadui wao. Kwa mfano, Yesu alimwambia mtume Petro: “Rudisha upanga wako mahali pake, kwa maana wote wanaochukua upanga wataangamia kwa upanga” (Mathayo 26:52).

Neno linasema wapendeni maadui, waombeeni mema wanaowauza. Hakuna mafanikio bila maadui. Maadui wanafanya uongeze kiu ya kutaka. Maadui wanakufanya usibweteke wakati huna kitu. Maadui wanafungua akili yako. Maadui wanakufanya ukimbie badala ya kutambaa. Maadui wanakufanya uone yale yasiyoonwa na wengi. Maadui wanasababisha ulipotakiwa ufike miaka 20 ufike kwa miaka 2. Maadui ni njia ya kufikia hatma yako: hakuna Samweli bila Penina (1Samweli 1:7-8, 20). Penina alikuwa anamchukia Hana. Akampa Hana upenyo wa kumzaa Samweli. Tuwapende adui zetu.

Nawe pia, uwapende adui zako katika maisha yako ya kila siku. Maana wote wanaochukua upanga dhidi ya adui zao wataangamia kwa upanga.
Biblia inasema kwamba tumtendee adui kwa fadhili, na kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunakusanya makaa ya mawe yanayowaka juu ya kichwa chake.

Hivyo, tukimwonesha fadhili mtu anayetuchukia, huenda tukayeyusha hasira yake na kutokeza sifa zake nzuri.

Jaribu kutatua matatizo na adui zako kwa amani. Mwawachie Mungu kazi ya kushughulikia ukosefu wa haki.
 
Ili kuwatawala waafrika, wapelekee Dini pamoja na Elimu.

Wahubirieni, mpende adui yako kama unavyojipenda.
Sisi tutawaibia mali, tutawabeba utumwani, hawatatuchukia maana biblia itawapooza machungu ya mioyo yao
.....
Wapeni Elimu, ili wajigawe makundi wasiwe na Umoja kamwe. Aliesoma amdharau asiyesoma.
 
Mafundishk kama haya huwezi ya kuta kwenye dini ya shetani ala na pedophile wake.
 
Huyo Mungu Alishindwa na Kashindwa kumpenda Adui yake Shetani na kumsamehe, Badala yake katutupia sisi huyo shetani aje atese watu Duniani.!!!

Hivi huyo Mungu wako ana jielewa kweli?
 
Back
Top Bottom