Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kuna baadhi ya watu wanatumia changamoto zinazowakumba watoto wa kike kujinufaisha, pasipo kujua kuwa wanatekeleza vitendo vya ukatili wa kijinsia. Vishawishi kama vile vyakula (mfano chipsi), usafiri (boda boda na magari), na vingine vya aina hii vinatumika kuvutia na kudanganya watoto wa kike, jambo linalowadhuru na kuathiri mustakabali wao.
Umbali mrefu wa kufika shuleni umekuwa kikwazo kikubwa kwa wanafunzi, hasa watoto wa kike, ambao hukutana na hatari ya kushawishiwa na kudanganywa katika safari zao.
Hali hii inasababisha baadhi yao kukata tamaa na kuacha masomo. Wengine hupatwa na changamoto kama mimba za utotoni na ndoa za mapema, jambo linalokatisha ndoto zao za kielimu.
Soma, Pia: Wanaume wanaweza kushiriki vipi katika Kampeni za Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Wasichana?
Jamii inawajibu mkubwa wa kutafakari na kuchukua hatua ili kukabiliana na changamoto hizi kwa watoto wa kike. Hii ni pamoja na kuongeza ulinzi kwa wanafunzi wanaosafiri kwenda shule na kuhakikisha wanapata mazingira salama ya kutimiza malengo yao ya elimu.
Aidha, wazazi wana jukumu muhimu la kufuatilia mienendo ya watoto wao ili kuwasaidia kukwepa hatari zinazoweza kuathiri mustakabali wao.
Soma: Mwaka 2023 kulikuwa na Makosa 37,448 ya Ukatili wa Kijinsia Tanzania, 15,301 yalikuwa kwa Watoto