tafsiri ya kiswahili ni mtaalamu aneyechunguza kifo cha mashaka ( duh ) sijui kama niko sahihi kwa mfano mtu amefariki kwa sababu ambazo sio za kawaida ( unnatural) na polisi katika uchunguzi wao wanashindwa kulink kifo hicho na au hawataki kumpeleka mtu mahakamani kutokana na kifo hicho watu waliotajwa kwenye post namba mbili wanaweza kuanzisha proceedings kuhusiana na kifo hicho.
Mfano halisi na mzuri ni wa watu waliokufa nyamongo, wale watu hawakufa kifo cha kawaida, walipigwa risasi basi ni lazima kuna mtu alipiga hizo risasi huyo mtu aliyepiga hizo risasi anatakiwa kupelekwa mahakamani. Kwa sababu polisi, kwa sababu wanazozijua moja hawataki kuwapeleka mahakamani basi hapo ndipo uchunguzi wa vifo hivyo inabidi ufanywe na coroner na chombo kinachosikiliza kinaitwa coroners court na mwenendo wote unaitwa inquest.