Kuwatangazia Oparesheni Panya Road hadharani ni kuwaogopa

Kuwatangazia Oparesheni Panya Road hadharani ni kuwaogopa

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Kuwatangazia panya road oparesheni ni kupeleka salamu ya kushindwa!

Ilitakiwa tutangaze tumefinya panya road wangapi hadi sasa!

Wakati mwingine kutangaza hadharani kwamba unaenda kufanya hiki na kile kutokomeza panyaroad.

kuwa makini na wanaokupigia makofi kwenye kikao hicho huenda kukawemo wafadhili wa panya road!

Kuwatangazia opareshenj ni sawa na kumeza dawa ya maumivu kwa muda ilihali ugonjwa unaendelea!

Kama tunaogopa kuwapiga risasi kwasabu za kidiplomasia basi tufanye yafuatayo! Mchawi mpe mwana akulelee!

  • Makempu yote ya vijana yasajiliwe! Kuwe na tamasha za vipaji kutoka kwenye kempu za vijana (michezo na burudani mbalimbali)
  • Kazi za periodic maintenance kutoka Tarura au manispaa mfano, kufyeka barabara wapewe hawa vijana waliosajiliwa kwa utambuzi.
  • Pamoja nakuwapa hizo tenda za usafi, pia semina iendelee waelimishwe na waambiwe kuwa wao ni sehemu ya ulinzi shirikishi! (Watalisaidia jeshi kulinda maeneo yao)
  • Makamanda wa mikoa na wilaya waambie wazi kwamba kukitokea uhalifu maeneo yao wahesabu hawana kazi
 
Matumizi ya neno "Panya Road" ni ya kujidhalilisha.

Msamiati huo au maneno hayo yamejikita kwenye ubaguzi wa kimbari. Ni lugha yenye hila zenye uasi katika jamii za Mwafrika.

Tuwe makini.
 
Back
Top Bottom