Kuweka engine ya 1KZ kwenye Land Rover Discovery

Chief

Platinum Member
Joined
Jun 5, 2006
Posts
3,588
Reaction score
3,194
Land Rover Discovery ni gari ambayo nzuri sana kwa ndani na bei yake si kubwa sana. Tatizo kubwa ni kwamba engine yake mara nyingi huwa ni za petroli na ni engine kubwa ambazo gharama za mafuta inakuwa juu sana.

Nimeona gari nyingi za Benz saloon zikiwekewa engine ya Toyota Mark II, na Pajero zikiwekewa engine ya 1KZ. Vile vile nimeona Land Rover Freelander zikiwekewa engine ya Rav4. Ningependa kujua kama kuna fundi Dar ambaye anaweza kufanya conversion hii, zaidi sana kama ataweza kubadili engine tu bila gearbox. Kwa akili yangu ndogo, atumie control box (ECU) ya 1KZ kuendesha engine na atumie control box ya Landrover kubadli gear na kuendesha suspension system yote kwa ujumla.
 
Ni kuchakachua kwa kwenda mbele, yaani body ni Benz lakini engine Toyota! Ubunifu mzuri sana!
 
Ukichukuklia bei ya spares za benzi ziko juu na mafundi wachache wa kuringa, hakuna mbadala ila kuchakachua tu.
 
Kaizer, RRONDO, MANI, CYBERTEQ, TCleverly

Hii mimi binafsi sijawahi isikia wala kuiona ila yaweza kuwa sawa lakini kama angeweza kuweka 1hz au 1hd-fe ingeweza kuwa safi zaid sababu ya power
 
Last edited by a moderator:
Kaizer, RRONDO, MANI, CYBERTEQ, TCleverly

Hii mimi binafsi sijawahi isikia wala kuiona ila yaweza kuwa sawa lakini kama angeweza kuweka 1hz au 1hd-fe ingeweza kuwa safi zaid sababu ya power

1HZ ni engine imara sana ila nadhani ni kutoitumia ipasavyo kuikiweka kwenye bodi ya Discovery. 1HD-FE hapo ndo power zaidi ila ni kurudi kule kule ninapokwepa, yaani fuel cost. Vile vile, kutokana na ukubwa wa hizi engine, inaweza zisi-fit kwenye engine bay ya Discovery. Engine swap inafanyika sana hapa Bongo betweeen the same make na different makes.
 
Kaizer, RRONDO, MANI, CYBERTEQ, TCleverly

Hii mimi binafsi sijawahi isikia wala kuiona ila yaweza kuwa sawa lakini kama angeweza kuweka 1hz au 1hd-fe ingeweza kuwa safi zaid sababu ya power

issue iko kwenye matairi huku mbele na kule nyuma....hizi discovery mara nyingi zinatumia vimikono vidogo kama drive shaft flani ndio maana unaziona zimekaa chini na hizi 1kz zinatumia tradition differential hivyo itabidi abadili vitu vingi sana...kwasababu ni lazima ubadili engine na gearbox complete

benz,bmw kuwekwa engine za 1g ni rahisi...wanabadili engine na gearbox complete...bmw/benz/mark 2 zote ni rear wheel drive kwahio kazi sio kubwa sana ni kukata na kuunga mikono ya diff. precisely
 
Land Rover Discovery ni gari ambayo nzuri sana kwa ndani na bei yake si kubwa sana. Tatizo kubwa ni kwamba engine yake mara nyingi huwa ni za petroli na ni engine kubwa ambazo gharama za mafuta inakuwa juu sana.

Nimeona gari nyingi za Benz saloon zikiwekewa engine ya Toyota Mark II, na Pajero zikiwekewa engine ya 1KZ. Vile vile nimeona Land Rover Freelander zikiwekewa engine ya Rav4. Ningependa kujua kama kuna fundi Dar ambaye anaweza kufanya conversion hii, zaidi sana kama ataweza kubadili engine tu bila gearbox. Kwa akili yangu ndogo, atumie control box (ECU) ya 1KZ kuendesha engine na atumie control box ya Landrover kubadli gear na kuendesha suspension system yote kwa ujumla.

mkuu,lazima ubadili engine na gearbox complete....pia differential ya L/ROVER na IKZ ni tofauti,landrover disc wanatumia mikono mifupi kama drive shaft fulani na ikz toyotas wanatumia traditional differential yenye mtungi kwahio kuna vitu vingi sana vya kubadili na kukata na kuunga miguu ya mbele na nyuma.

european car nyingi zina control box mbili...ya engine na ya vitu vingine vya gari...wanaobadili engine huwa wanaweka control box ya toyota inarun engine na ile ya vitu vingine vya gari inabaki hivyo hivyo.

kwahio hapa lazima ununue
1.gearbox ya toyota
2.engine ya toyota
3.differential ya toyota na axle zake
4.control box ya toyota kwa ajili ya engine tu[vitu vingine inabaki moja ya hio discovery]
lazima uwe na fundi umeme mkali sana ku-link hizo control box mbili

kuna fundi yuko kinondoni nilishuhudia akibadili bmw engine na kuweka 1g ni fundi mzuri sana bahati mbaya namba zake nimepoteza.

USHAURI WANGU: kama discovery ni V8 na unaogopa wese tafuta engine yake TD5,TDV6 weka nakuhakikishia itakuwa cheap na less headache kuliko kubadili kila kitu
 
issue iko kwenye matairi huku mbele na kule nyuma....hizi discovery mara nyingi zinatumia vimikono vidogo kama drive shaft flani ndio maana unaziona zimekaa chini na hizi 1kz zinatumia tradition differential hivyo itabidi abadili vitu vingi sana...kwasababu ni lazima ubadili engine na gearbox complete

Mi sio fundi ila natumia akili ya kawaida tu. Ingawaje differential ni tofauti, lakini zote zinazungushwa na propeller shaft. Sasa kwa nini nibadili differential wakati haijalishi propeller shaft inazungushwa na engine gani? hata hivyo, ndio maana nikapendekeza kuwa engine tu ibadilishwe na sio gear box. Hapo inahitajika fundi mzuri sana wa umeme wa magari kama ulivyosema.
 
Kaizer, RRONDO, MANI, CYBERTEQ, TCleverly

Hii mimi binafsi sijawahi isikia wala kuiona ila yaweza kuwa sawa lakini kama angeweza kuweka 1hz au 1hd-fe ingeweza kuwa safi zaid sababu ya power

inawezejana sana, sema mimi sijamwelewa, gari tayari analo na linamsumbua au ndiyo anataka kununua!! tatizo watanzania tunaangalia soko moja tu, Japan! uk zimejaa za diesel 2.7L kwa nini uagize japan?
 
Ndio maana nikapendekeza kuwa engine tu ibadilishwe na sio gear box. Hapo inahitajika fundi mzuri sana wa umeme wa magari. .

engine na gearbox lazima ziwe zimepimwa zilingane....ukiweka gearbox ya toyota kwenye discovery inaweza ikashindwa kuhimili msukumo wa engine na speed ikapasuka......huwezi kumix hebu fikiria clutch plate/pressure plate/flywheel ya toyota itafit vipi kwenye engine ya discovery?? ni tofauti sana.

wote wanaobadili engine wanabadili na geabox ni lazima unless iwe 1kz kwa 1kz au discovery kwa discovery
 
issue iko kwenye matairi huku mbele na kule nyuma....hizi discovery mara nyingi zinatumia vimikono vidogo kama drive shaft flani ndio maana unaziona zimekaa chini na hizi 1kz zinatumia tradition differential hivyo itabidi abadili vitu vingi sana...kwasababu ni lazima ubadili engine na gearbox complete

benz,bmw kuwekwa engine za 1g ni rahisi...wanabadili engine na gearbox complete...bmw/benz/mark 2 zote ni rear wheel drive kwahio kazi sio kubwa sana ni kukata na kuunga mikono ya diff. precisely

diff na gearbox mbona hapo havikutani?

MF: ENGINE+GEARBOX+PROPELA+DIFF***.
NI HIVYO MFANO HALISI.ILA UNAWEZA KUBADILI FRENCH 1 YA PROPELA ILI INGILIANE NA GEARBOX.
 
Braza lazima ubadilishe gearbox sabab kila engine ina rpm yake yan revolution per minute mfano engine yeny piston nying inauwezo wa spin faster than yenye piston chache hata kama zitakuwa na cc sawa

hvo ucpobadilisha hautapata spid inayotakiwa
 
inawezejana sana, sema mimi sijamwelewa, gari tayari analo na linamsumbua au ndiyo anataka kununua!! tatizo watanzania tunaangalia soko moja tu, Japan! uk zimejaa za diesel 2.7L kwa nini uagize japan?
Bei za UK ni kubwa kulinganisha na Japan (C&F). Halafu hakuna dealers wengi toka UK ambao wana-ship outside Uk, (uelewa wangu) na vile vile spares za Toyota ni rahisi sana kupata/bei kuliko Discovery. Sijanunua hii gari ila nina wazo la kufanya hivyo kama idea hii inawezekana.
 
diff na gearbox mbona hapo havikutani?

MF: ENGINE+GEARBOX+PROPELA+DIFF***.
NI HIVYO MFANO HALISI.ILA UNAWEZA KUBADILI FRENCH 1 YA PROPELA ILI INGILIANE NA GEARBOX.

diff inaungana na prop then gearbox....prop/gbox ya disc ni tofauti na toyota hapo ni either uibadili au ukate then uunge kipande cha mbele na nyuma ambayo inaewza kusababisha vibration...mind u gari ni 4wd so kuna matairi ya mbele pia.
 
Bei za UK ni kubwa kulinganisha na Japan (C&F). Halafu hakuna dealers wengi toka UK ambao wana-ship outside Uk, (uelewa wangu) na vile vile spares za Toyota ni rahisi sana kupata/bei kuliko Discovery. Sijanunua hii gari ila nina wazo la kufanya hivyo kama idea hii inawezekana.

kama hujanunua nunua la diesel tu wala spares sio issue sana.
 
Braza lazima ubadilishe gearbox sabab kila engine ina rpm yake yan revolution per minute mfano engine yeny piston nying inauwezo wa spin faster than yenye piston chache hata kama zitakuwa na cc sawa

hvo ucpobadilisha hautapata spid inayotakiwa
Hiyo ni sababu ya msingi kabisa ya kuifikiria. Ukiangalia hapa utaona kuwa maximum RPM ya 1KZ ni 6000 na hapa maximum RPM ya 94D ya Discovery ni 6000. Hivyo, kwa nadharia tu gearbox ya Discovery itafanya kazi vizuri kwa engine ya 1KZ.
 
Rpm ni kitu kikubwa xna cha kuangalia la sivyo utakuta umepanga gia zote rpm iko mwisho afu spid labda 120
 
Bei za UK ni kubwa kulinganisha na Japan (C&F). Halafu hakuna dealers wengi toka UK ambao wana-ship outside Uk, (uelewa wangu) na vile vile spares za Toyota ni rahisi sana kupata/bei kuliko Discovery. Sijanunua hii gari ila nina wazo la kufanya hivyo kama idea hii inawezekana.

nimekusoma mkuu! lakini dealers ni wa kumwaga, hata hao wajapan sku hizi wanasource mpaka uk, jaribu tu kuongea nao uwaambie mahitaji yako usiangalie magari yaliyo kwenye stock list tu. otherwise nunua toyota tu isije kukusumbua baadaye ukaonaumepoteza pesa za bure!
 
Back
Top Bottom