Kuweka uso/face/ sura ya/wa mtoto kwenye social media. Nini madhara yake

Kuweka uso/face/ sura ya/wa mtoto kwenye social media. Nini madhara yake

Doto12

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2023
Posts
787
Reaction score
1,394
1000288876.jpg
Hii tabia ya kuwaweka watoto wadogo kwenye mitandao ya kijamii(social media) Facebook Instagram nk nk
hii ni tabia mbaya sana. Ni kawaida kuwaonyesha watu damu zetu, uzur wetu lakini sio sawa.

Yeyote aliyemuweka mwanae kwenye hii mitandao, na hata Whatsapp mnawekwa sio busara.

Ule uzao wako, bado unahitaji ulinzi, ikiwa unapenda kupiga picha mwanao zitunze hadi akikua aone alikuwaje angali mtoto, ataona alikuwa cute au alikuwa kawaida. Katika sura ya utoto hakuna uhalisia utakuwa hivyo jkubwani, hivyo ni kuudanganya umma na wewe mwenyewe.

Yapo macho manaya na wapo wenye nia mbaya, ikitokea wamemuhusidu mwanao utayavaa matatizo au hata kumkosa mwanao.

kwa mfano nimeshuhudia kijana mmoja amesoma akamaliza chuo na jeshini ameenda lkn hiv sasa yu kijijini anaendeleaha toroli. Siwez kusema moja kwa moja chanzo.

Kifupi tunawadhalilisha, hawajui, hawana uelewa ni majaaliwa ya mungu tu anawalinda malaika wake.

1000288874.jpg
Ieleweke kwamba muonekani wa utotoni sio atakuwa hivyo ukubwani. mfano. Hamisa mobeto alivyo sasa sivyo alibyokuwa akiwa na miaka 7, 13, 18 na kadhalika. kwa hiyo kuonyesha picha za nyakati hizo ni kuuhadaa umma na wew mwenyewe.

1000288872.jpg



Tuwaondoe watoto kwenye mitandao maana si heshima kwa mtoto na hawezi kujitetea.

Zipo baadhi ya jamii, huwezi kumuona mtoto wake, mfano waarabu, wahindi mtoto hutamuona kirahisi majiani au nyumbani kwake. Kwenye mitandao jamani tunafika mbali sana.

Hembu sasa tuone madhara yake.
Baadhi ya jamii huamini kwamba kuonesha mtoto sana hadharani kunaweza kuvuta wivu au husuda kutoka kwa watu wenye nia mbaya kiroho.

Watoto huchukuliwa kama zawadi au baraka. Kuwaweka wazi kupita kiasi kunaweza kuonekana kama kutohifadhi heshima na thamani yao ya kiroho.

Mtoto akizoea kusifiwa sana hadharani anaweza kukua na tabia ya kutegemea sifa za watu badala ya maadili ya ndani.

Baadhi ya imani zinaeleza kuwa mazingira ya wazi yasiyo na mipaka (kama mitandao ya kijamii) yanaweza kufungua milango ya ushawishi mbaya wa kiroho au maadili.

Katika tamaduni nyingi, wazazi wana jukumu la kulinda watoto wao kimwili na kiroho. Kuwaweka wazi bila tahadhari huonekana kama kupunguza ulinzi huo.

Mitandao ya kijamii mara nyingi hujikita kwenye umaarufu na kuonekana. Hii inaweza kuathiri ukuaji wa kiroho wa mtoto kama atajifunza kutafuta thamani yake kupitia sifa za watu badala ya maadili, imani, na tabia njema.

Mwisho kila mtu ana imani yake hivyo sio lazima ila muhimu zaidi ni kuhakikisha mtoto analindwa kimwili, kisaikolojia, na kiadili.
 
sasa mkuu fano mtu anacontact 30 hapo "wasapu" akiweka picha ya mtoto, na mtaani kuna watu majirani kaya 30 --- hivi sio ngoma droo hii mkuu?

japo nakuunga mkono hii tamaduni ya kujipost hata mimi siielewi kabisa
 
sasa mkuu fano mtu anacontact 30 hapo "wasapu" akiweka picha ya mtoto, na mtaani kuna watu majirani kaya 30 --- hivi sio ngoma droo hii mkuu?

japo nakuunga mkono hii tamaduni ya kujipost hata mimi siielewi kabisa
jamii za watu wengine wana ushamba huu wa kupost watoto wao?
 
Huwa n ulimbuken wa watu kupost watoto wadogo hasa fb Instagram wengi wao unakuta wamejua smart phone ukubwani
 
Achaa waendelee kupost na hao watoto wakikua waendelee kusema kizaz kimebadilika ila ukwe watoto hulindwa kwa kuwaficha na si kila mt anapaswa kumuona au kuwashika ovyo watoto
 
jamii za watu wengine wana ushamba huu wa kupost watoto wao?
sijafahamu mkuu,
ila wao wakianza kufanya hivo kuanzia kesho (ikiwa hawakua wakifanya) vipi ndo itakua standard/reference
?
 
Back
Top Bottom