Mzalendo, asante kwa maswali na hoja zako za ziada. Nitazifafanua kama ifuatavyo.
Maelezo yako yamenifanya niibue swali lingi. Je kwa nini TPN pamoja na kuwa na kurugenzi au idara nyingi lakini inachukua muda mrefu sana kutake-off. Mpaka sasa kwenye website yake inaonekana TPN ni NGO inayoandaa makongamano tu. Sasa wengi wetu tungetaka kujiunga na body inayowawezesha watu kuinvest practically ikiendana sambamba na makongamano kwa ajili ya nadharia lakini msisitizo uwe kwenye vitendo. Wasiwasi wangu hasa ni kwamba diaspora itakuwa slow kwenye kujiunga na NGO ambayo action zake zote ni makongamano.
.
Kama ulifuatilia mijadala yaTPN, utagundua kuwa TPN ilianza rasmi July 2007. Na napenda nikujulishe kuwa kuna mafanikio mengi sana ambayo tayari yamepatikana. Mafanikio hayo si ya Ngonjera au ya kisiasa bali ya vitendo. Tafadhali rejea:
https://www.jamiiforums.com/matanga...-karibuni-tanzania-professionals-network.html
na
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...nzanians-diaspora-summit-december-2009-a.html
Kwa maelezo ya kina na mafanikio kisha nijulishe kama bado utahitaji maelezo ya ziada.
Mimi niko tayari kujiunga na TPN (kama nilivyoahidi siku za nyuma) lakini najiuliza mwezi mmoja baada ya kujiunga nitanufaika vipi, miezi miwili, mwaka mmoja , miwili, mitatu baada ya kujiunga TPN itaniwezesha vipi kuwa katika better position??? Hivi ni vitu vya msingi kuviweka bayana ili diaspora iwe tayari kujiunga.
Unayozungumza ni ya kimsingi na ndiyo Changamoto kubwa. Wengi wanataka kujiunga ili wafaidi moja kwa moja. Tuliopo sasa tunawajibika kujenga mazingira hayo kwa TPN kujijengea uwezo katika maeneo mablimbali ya msingi. Wachache tuna mawazo ya "What Can We Do For Our Country" and not the opposite way. Hata hivyo napenda kukufahamisha kuwa tayari tuna members wengi ambao ni Diaspora na kama nilivyodokeza tayari tuna Chapter UK na USA, unaweza kuwasiliana nami nikakupatia contacts kama uko maeneo hayo.
So Mkuu, be specific na nina uhakika TPN itakusaidia. Research tuliyoifanya huko nyuma inaonyesha kuwa matatizo yetu ya Kujiwezesha Kiuchumi ni ya namna tatu:
- Maarifa ya Ujasiliamali - TPN inatoa Elimu
- Mitaji - TPN ina model ya kuwaunganisha members wapate mitaji na kuwapa access ya Mikopo. Pia TPN sasa ina Fund.
- Masoko - TPN ni mtandao na katika huo mtandao tunautumia pia kama Market Place na Networking (Its like Jamatini thing but much better).
Kama una mawazo ya kuboresha zaidi, tunakukaribisha tuendelee kushauriana.
Kwenye website haielezewi bayana ada ya kujiunga ni sh. ngapi, ila kama sikosei nilipata ambiwa kuwa membership fee ni sh. laki moja kwa mwaka. Sasa kwenye list ya wanachama nimeona majina 505, which means that kila mwaka TPN inakusanya sh. milini 50 kama ada za wanachama. Hiki kiasi kinatosha kuiwezesha TPN kuwa na activity inayoonekana kila siku.
Baada ya kupitia majina ya members wake tathmini yangu ni kwamba TPN ina potential kubwa kuliko jinsi inavyoperfom.
Kama nilivyodokeza, TPN website inatengenezwa upya na itakuwa na Information zote muhimu. Tunaomba uvumilie kidogo tu.
Kuhusu fees, zilifanyiwa marekebisho kwenye last AGM. Registration ni TZS 50,000 na Monthly Subscription ni TZS 10,000. Kinadharia TPN ina members na Wapenzi zaidi ya Million 5. Hata hivyo walioko katika list kwa sasa ni zaidi ya 1000.
Tunakubaliana na wewe kuwa TPN ina potential kubwa sana na hilo tayari tunaliona kutoka katika yanayotokea sasa hivi. Tungependa kukua kwa uhakika na kujenga mfumo wa mageuzi halisi ya kiuchumi kuanzia kwa mtu binafsi. Bado kazi ni kubwa lakini naamini kwa dhamira na utashi tulionao, tutafika.