Kuweni makini, Global Financial Crisis (Mtikisiko wa uchumi) is coming and real

Kuweni makini, Global Financial Crisis (Mtikisiko wa uchumi) is coming and real

Teslarati

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2019
Posts
2,621
Reaction score
10,466
Kuna mitikisiko midogo midogo ya uchumi huwa inatokea na inadumu kwa muda mfupi lakini kuna ile mikubwa kama Great Depression, hii mikubwa yote huwa inatanguliwa na vita pamoja na utra super overspending kuanzia level ya watu binafsi, familia, makampuni hadi nchi kwa ujumla.

Nikisema ultra super overspending namaanisha matumizi ya juu kupitiliza yaliozidi kiwango. Na hayo husababisha watu/makampuni/nchi kuchukua mikopo ambayo baadae inakua ngumu kurudisha. Mikopo hio inaweza chukuliwa ili ku-finance vita, expansions, etc....

Sasa mwaka juzi katikati hadi mwaka jana tulishuhudia mtikisiko wa uchumi ambapo wataalam wengi walidhan utaisha na 2024 itakua njema, lakini kwa indicators ninazoziona na kusimuliwa, aisee 2024 will be the worst of 2020s. Yaani itakua mbaya zaidi ya 2020, 2021, 2022 na 2023.

Makampuni makubwa ya nchi zinazoongoza uchumi yako hoi. USA kila siku wanafukuza kazi watu japo miaka ya nyuma walifukuza pia, China napo hali ni mbaya saaana, china hakufai kabisa hivi ninavyoongea. Europe ambao wanamtegemea kaka yao US wao wameshazoea uchumi mmbovu unaozidi kuanguka tu kila siku.

Wadau wekeni savings, na fanya diversification ya savings zako sababu kuna muda unaweza fika hata bank wakakwambia unaruhusiwa kutoa mwisho 1m tu kwa wiki.
 
Back
Top Bottom