Kuweni makini na bidhaa za WESTPOINT

mimi Mbona nimenunua fridge na Brenda huu mwez wa 9 Mbona havisumbui?Kwan haukupewa warrant?au umenunu Kwa mtu

Mi pia nimenunua fridge, blender, toaster, fan mwaka wa 4 na havina matatizo...
 

Mkuu mimi naona bidhaa hizo ni fake - Westpoint ina-manufucture bidhaa za high quality, lakini kuna makampuni fake kutoka Far East zinatengeneza white goods hizo alafu wanaweka NEMBO za Westpoint, Hotpoint etc, hata India wanafanya ujanja huo - Dubai inatumika sana kueneza bidhaa hizi fake kwa nchi za Africa Mashariki, wafanya bihashara wabongo wanalijua sana hilo actually wanashilikiana nao katika mchezo huo hatarishi.

Mkuu TBS wana mahabara za kuchunguza bidhaa kama hizo, tatizo ni kwamba hawafanyi kazi zao kwa uhaminifu.
 
Nakubaliana nawe kabisa! Sijui hata FCC wanafanya nini! Mtu akishapewa mamlaka kazi inakuwa kula na kuhudhuria vikao ili apate posho.
 
Hizo bidhaa nafikiri ni fake! Mimi nilinunua deep freezer lina miaka zaidi ya kumi linadunda vizuri sana na wala sijajaza gesi kwa muda wote huu!
 
Mimi sitaki kusikia kitu kinaitwa Westpoint. Nilinunua friji la Westpoint Top Shop miaka kama mitano iliyopita, nilisumbuka sana mpaka nikaamua kumsusia mwenye duka. Ilikuwa ni gharama za kulipeleka kutengenezwa na kulirudisha nyumbani mpak nikachoka nikalisusa.
 
Mimi friji langu nililonunua mwaka 2011 kutoka wakala wa westpoint limehamribika. linawaka lakini halipoozi. Hawa jamaa siwaamini tena.
 
Nina friji ya Westpoint toka 2008, imedumu mpaka inaniuzi.
 
Nunua kitu Hitachi. Nilinunua mlimani city miaka minne inapiga mzigo bila shida.
 
Naunga mkono hoja, mimi rice cooker nilinunua hata miezi 6 haijaisha waya zinang'oka
 
Niliwahi kununua blender ya westpoint nilikaa nayo wiki chache sana ikaharibika.
Sikuwa na time ya kuipeleka kituni kwao.
 

Ahaa haaaa haaaa .... leo ni mwaka 2019, bado inaendelea kupika kazi kama kawa, halijawahi kusumbua ama kuzimwa zaidi tu pale TANESCO wanapofanya yao. Zaidi ya muonekano kufifia, sijawahi hata kuongeza gas ....
 
Hao westpoint bidhaa zao zilikiwa ni zamani kuanzia mwaka 2010 kurudi nyuma sisi tuna friji na tv chogo na mpaka sasa vinapiga kazi tv haijawahi hata kufunguliwa ila friji tuu ndo imeongezwa gass tena mara 1
 
West Point ni kampuni ya kifaransa.

Wachina wametengeneza bidhaa feki wamezileta Afrika.

Kwahiyo westpoint zinazokuja afrika ni feki.
 
Nina friji ya West Point tangu 2008 hadi leo sijaongeza gas wala kuharibika kitu chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…