Kuweni makini na facebook

Kuweni makini na facebook

globalization inapokuja huja na effact zake
 
Sidhan kama uchafu alioufanya huyu mwanamke unaweza kuhusishwa na facebook..hii ni tabia ya mtu tuu hata asingetumia facebook kama ni tabia yake na alidhamiria kucheat facebook isiwe kigezo. halafu huyo mwanamke anaenekana ni wale wale mama huruma..ambao hawajui kusema No. Pia umri wa huyu mwanamke unatakiwa uangaliwe..labda alidanganyika kwa kutokuwa na uelewa au upeo wa kujua jambo alilofanya la aibu na fedheha sana. Hivi ndani ya mwezi tuu umefahamiana na mtu tena kwenye social network na tayari umekuvulia kufuli?? na tena cha kusikitisha ni mjamzito!! nadhan jamaa anatakiwa afanye uchunguzi wa kina kuhusu huyo ujauzito, huenda ukawa na kasoro, kama mwanamke anaweza kucheat akiwa na mimba tena kwa mtu aliemfahamu kwa kipindi kifupi sana..je kwa wale wanaofahamiana kwa muda mrefu si ni tatizo..hata week haitaisha jamaa atakuwa ameshalamba joker! kwa ufupi ni kwamba hii tabia ya huyo mwanamke na sio kwa vile alitumia facebook. facebook haikumpa mbinu au facebook haikumlazimisha mwanamke atoke na jamaa. Facebook imeleta mafanikio wa wengi ambayo wameitumia ipasavyo na sio vinginevyo.
 
Back
Top Bottom