Hakuna mtu yyte bongo narudia tena BONGO mwenye uwezo wa kusikiliza mawasiliano ya whatsapp au telegram hata kama mtu unatumia tecno y3...
Unajifariji kiongozi.
Umesahau kama nchi ile iliingia mkataba na Israel wa ushirikiano mambo ya usalama na taarifa za intelijensia.
Hiyo whatsap inafanya end-to-encryption na hiyo inasaidia ku-secure message wakati inasafirishwa. Inapoingia tu ktk kifaa chako inakuwa deciphered(decoded) kuwa plain text au kuwa normal un-encrypted voice or video message, ndio maana wewe unaweza kusoma text au kusikia voice au kuona video halisi.
Kwahivyo yeyote ambaye anaweza kudukua kifaa chako ataweza kupata access ya hizo apps au tuite services kama vile wewe unavyo zipata zikiwa decoded.
Je inawezekana kudukuliwa kifaa chako na wenye nyenzo au miundombinu sahihi?
Jibu ndiyo.
Mfano: Jiulize mamlaka fulani ile inajuaje simu flani imekuwa hacked au cracked na kubadilishwa IMEI?
Mamlaka au mitambo ya mitandao ya simu inajuaje ume crack modem kiasi kwamba ukiitumia tu hiyo modem muda mfupi inakukatia mawasiliano?
Je mara ngapi umepokea configuration message za internent kwenye device yako na ukakubali ku-install?
Unajuaje kama ktk hizo message wali emmbed spyware kama vile mfano wa PEGASUS?
Hiyo ni mifano ya michache na haimaanishi nipo sahihi au imetokea hivyo.