Tetesi: Kuweni makini na VAR toka Israel, Musiba anajua kibanda cha VAR kipo wapi


Hiyo PEGASUS imenunuliwa sana na nchi kadhaa khasa za huku kwetu.
 
Kwenye audio kadhaa sauti ya Nape inasikika zaidi kuliko wenzake, means kuna wasiwasi yeye ndo aliekua akirekodi.

Sifahamu ni kwanini Nape ameshindwa kumshauri rafiki yake January Makamba na wazee Makamba na Kinana kuhusu hili suala zima la waraka.

Mzee Pius Msekwa yeye karuka mita 100 ametulia anatazama.
 
 
Wabishi mtanielewa tu nilikuwa naandika nini someni hiyo habari chi :-
WhatsApp yalishitaki Shirika la Israel kwa kufanya udukuzi wa mawasiliano ya Wanahabari na Watetezi wa Haki za Binadamu
 
Na uvumbuzi mkubwa wa karne uliofanywa na Google ule wa computer yenye nguvu sana (Quantum Computing Supremacy)
ndio unakuja kurahisisha kazi ya kudukua.

Kutakuwa hakuna encryption ambayo itaishinda computer maalum kama hiyo.

Fikiria Google Quantum Computing Processor inaweza kufanya kazi kubwa sana kwa sekunde 200 tu kazi ambayo hadi sasa hufanywa kwa miaka 10,000 au zaidi na Super computer inayo ongoza kwa computing power kwa miaka mingi iliyotengenezwa na IBM.
Hello quantum world! Google publishes landmark quantum supremacy claim
 
Kama watakua wanamdukua Sky eclat, deceiver, Faizafoxy, titicomb, zito kabwe, mwamba, mshanajr. N.k watakua hawakitendei haki hicho kifaa.
Kuna wakuu wengine mnadhani kutaja jina Bar shit, korodanimije ni upinzani
 
Boss apo swali langu ni kwamba
Kama wanasubiri sms au voice note ifike ndo waidukue je, wanaweza kufuatilia online voice call or video call?
Nawasilisha..
 
Boss apo swali langu ni kwamba
Kama wanasubiri sms au voice note ifike ndo waidukue je, wanaweza kufuatilia online voice call or video call?
Nawasilisha..
Haisubiriwi kitu, kikishadukuliwa kifaa chako wanaona na kusikia kila kitu.
Kibaya zaidi kifaa chako kinatumika kusambaza kirusi wa kudukua watu wote unaofanya nao mawasiliano au walio ktk contacts za kwenye device.

Kinachofanyika wanadukua na kukiteka kifaa chako, wanakuwa kama wamekishika wao kama vile unavyokuwa unakitumia wewe.

Kila kitu kiwe online au offline(wanaweka software ya kurekodi vitu, ukiwasha tu internet boom!wanapitia mzigo uliokusanywa offline), kiwe live stream au vyovyote vile.
Kifupi wanaweza hata kumpigia video call mpenzi wako wakapachika sura yako kisha mwenzio akajiachia kwavile anaonadhani anakuona wewe live.

Hizi enzi za 3D printing wanaweza kutengeza sura yako ya bandia ya plastiki akaivaa mtu na sauti yako ikagushiwa.
Kumbuka unazungumzia unafuatiliwa na watu/taasisi wenye/zenye rasilimali(resources) za kutosha iwe fedha, teknolojia na watu.
 
Whatsapp na Telegram ni salama vinginevyo mengi yangejulikana
Wanaodukuwa mawasiliano ya Whatsup na Telegram hawaidukui program yenyewe per se! Wanaingilia simu yako na kuiteka wanakuwa na access nayo kama wewe mwenye simu. Hapo sasa ndiyo wanakuwa na access na hizo program kama wewe unavyoweza kuzitumia. Haya yote yanafanyika bila wewe kujua.
 
Boss apo swali langu ni kwamba
Kama wanasubiri sms au voice note ifike ndo waidukue je, wanaweza kufuatilia online voice call or video call?
Nawasilisha..
Wanaweza kuwasha camera yako bila kujua wakakupiga selfie au kupiga picha ndani mwako n.k.
Unamkumbuka mchungaji/askofu flani maarufu toka Koromije na sex tape yake?

Inawezekana ilikuwa ya kweli na lipigwa picha bila kujua toka kwa webcamera ya laptop yake au alipigwa kwa simu yake ikiwa ktk charging stand.
 
Mkuu unachekesha kiasi flani.
Serikali ijenge flyover, madaraja kama ya Kigamboni, Ifakara, inunue ndege zote, RADAR za kisasa, mifumo ya BVR kisha ishindwe kununua hii huduma au software?
Hiyo nchi itakuwa ni mtaa tu sio nchi kamili.
 
Nawakumbusha wazayuni walitupa vifaa vya mawasiliano cjui vko kwa bashite au vilirudi Tc mcfkir mko huru kiasi hicho
 
Kurekodiwa kwa siri na chombo kilicho ruhusiwa kisheria ni kosa?
Au ushahidi wake ni haramu?

Kwanini telephone tapping/wire tapping, often by covert means inafanyika duniani kote hata huko marekani na taasisi kama NSA, FBI na CIA wanatumia hii njia na wanakamata watu kwa ushahidi huu na wanafungwa watu?
 
Nawakumbusha wazayuni walitupa vifaa vya mawasiliano cjui vko kwa bashite au vilirudi Tc mcfkir mko huru kiasi hicho
Wazayuni, pamoja na mkurugenzi wa Idara nyeti, na mkuu wa wakakamavu walitia saini ya ushirikiano ikiwemo kuuziana mitambo, ilikuwa pale makao makuu ya wakakamavu Upanga.

Haikuwa siri iliandikwa na kutangazwa na vyombo vya habari kibao sema watu wasahaulifu tu.
 
Hakuna kinachopotea kwenye Computer, kwa taarifa yako simu yeyote hasa smart phone ni computer kamili.
Operating system za Smart phone ni Unix based OS ka vile Linux, n.k.
Mimi niletee computer/simu yako futa unavyojua wewe kisha nakurudishia hivyo vitu.

Sasa jiulize itakuwaje hizo nyenzo za wazayuni?
Mimi kilaza tu kama wengine wengi.
 
Chombo chochote kinachokuwa controlled na mwingine hakina siri...
everything is for sale but for the right price....
 
Ile ya yule askofu ilidukuliwa kutoka kwenye simu yake au Laptop kama ulivyosema. Inaelekea ana mtindo wa kujirekodi na kuhifadhi hizo clips halafu anakuja kujiangalia baadae alivyokuwa anatenda. Sasa wajanja wakaingilia simu yake na kuitungua.Kuna mmoja anapinga eti hatuna fedha ya kununua. Naona anaota ndoto ya mchana. Ma -hackers wako wenye uwezo mkubwa sana. Nchi kama China, Urusi na Marekani kuna watu wenye uwezo mkubwa. Hao ukiwakatia chao wanakufanyia kazi unayotaka. Hapo sijazungumzia ushirikiano wa nchi na nchi au nchi na makampuni makubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…