Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Mapambano dhidi ya uhalifu wa mtandaoni yanaendelea. Tafadhali kaa chonjo na chunguzq mara mbili kila anwani ya barua pepe inayojihusisha na masuala ya kazi au interview haswa online interview.
Hii ni mahususi kwa wale ambao hupenda kutumia barua pepe, haswa Gmail.
Kwa zaidi ya miezi miwili sasa watu wamekuwa wakipokea barua pepe (email) kutoka kwa Emma Young na anwani yake wa barua pepe ni "[email protected]" hii ni barua pepe bandia.
Huyu Emma anadai kuwa yeye ni Senior Recruiter katika Kampuni ya Pulse Tree Recruitment, kitu ambacho ni uongo mkubwa, kwa lugha nyepesi huyu ni tapeli.
Kwa wale wenye uchu wa kupata kazi kuweni makini kitawaramba muda sio mrefu. Huyu Emma Young ameshawapiga watu huko duniani, na kampuni ya Pulse Tree Recruitment haimtambui hata kidogo na wao hawatumii anwani hiyo ya kitapeli bali hutumia anwani ya pulserecruitments.com.au ama pulsegroup.com.au pekee wala sio pulsetreeplacement.com hii kutoka kwa Emma Young.
Mwisho wa barua pepe wameandika hivi:
We respect your privacy. To be removed from our communication, click here to unsubscribe.
Kuna watu maeneo kadhaa walikuwa vichwa vigumu walikuta wamedukulia taarifa zao pasipo wao kufahamu.
MTU WANGU USIJE KUBONYEZA HICHO KIUNGO, USIBONYEZE HIYO LINK. CHA KUFANYA NI KUIACHA HIYO BARUA PEPE HUKO HUKO SPAM MESSAGES.