SoC02 Kuwepo na sera ya elimu nchini Tanzania yenye kuboresha na kutekelezeka kwenye vituo vinavyotoa elimu katika mfumo usio rasmi(tuition centers)

SoC02 Kuwepo na sera ya elimu nchini Tanzania yenye kuboresha na kutekelezeka kwenye vituo vinavyotoa elimu katika mfumo usio rasmi(tuition centers)

Stories of Change - 2022 Competition

Tonytz

Senior Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
159
Reaction score
1,142
Utangulizi
Sera ni matamko yatokanayo na masuala ya msingi yenye dhamira ya kuelekeza namna ya kukabili changamoto kwa ajili ya maendeleo katika jamii. Aidha, inaweka wazi dira na dhima na kuelekeza juu ya utekelezaji wa majukumu ya wizara, idara, taasisi, sekta binafsi na jamii kwa ujumla. Sera inazingatia Dira ya Taifa na mikakati ya maendeleo ya kitaifa na kimataifa. Wananchi ndiyo chimbuko, walengwa wakuu, wadau na watekelezaji wa sera. ( Sera ya Elimu na Mafunzo, 2010. Toleo jipya la mwaka 2011)

Kwa upande mwingine elimu isiyo rasmi ni elimu ambayo hujifunzaji wake hupatikana kwa njia isiyo na muundo, nje ya taasisi rasmi za elimu za jamii. Elimu hii aghalabu haifundishwi katika shule rasmi kulingana na miongozo ya mitaala inayoendelea ( Nukuu kutoka sw.warbletoncouncil.org)

Katika Makala hii nitajikita Zaidi katika kuzungumzia kwa ufupi sana sera ya Elimu nchini Tanzania katika jitiada za kuinua na kuimarisha vituo vinavyotoa mafunzo ya elimu kwa mifumo isiyo rasmi ambapo nitaangazia Zaidi kwenye vituo vinavyotoa elimu ya ziada (TUITION CENTERS), sera ya elimu na mafunzo( 2014) Dira na dhima yake, sheria katika sera ya elimu, faida kwa jamii na serikali endapo sera itavizingatia vituo vinavyotoa elimu kwa mfumo usio rasmi( tuition centers).

Miongoni mwa sera zilizotumika Tanzania baada ya uhuru ni Sera ya Elimu na Mafunzo(1995), Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo (1996), Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu(1999), Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Elimu ya Msingi ( 2007), na Sera ya Elimu na Mafunzo (2014).

Dhumuni la sera hizo ilikuwa ni kutoa mwongozo kuhusu kuongeza ushirikishwaji wa sekta binafsi, kuongeza fursa za elimu na mafunzo kwa usawa, kuimarisha uhusiano kati ya elimu rasmi na elimu nje ya mfumo rasmi na kuwezesha ukuaji wa utamaduni wa elimu ya kujiajiri na kubuni ajira. Dira ya Taifa ya maendeleo 2025 na Mpango wa Taifa wa maendeleo wa muda mrefu 2011/12 hadi 2024/25, serikali imelenga kujenga jamii iliyoelimika na yenye kupenda kujielimisha. Sera ya elimu ya 2014, sera hii iliweka Dira ya elimu na mafunzo nchini kuwa ni”Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mitazamo chanya ili kuweza kuchangia katika kuleta maendeleo ya Taifa” (sera ya elimu na mafunzo 2014)

Ukiangalia kwa undani ni dhahiri kuwa sera hii na nyinginezo ilitambua mchango wa elimu isiyo rasmi kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa letu. Lakini pamoja na kuwepo kwa sera na Dira hizo, je serikali au mamlaka husika inavipa kipaumbele vituo vinavyotoa elimu katika mifumo isiyo rasmi?

Ukiangalia matamko ya kisheria katika mifumo isiyo rasmi ya utoaji elimu yamekuwa ya kimaandishi Zaidi na siyo kiutekelzaji, kwani kama havina tija.

Mwanambugulu-JF-EXPERT MEMBER, 20/7/2019 “ELIMU ISIYO RASMI” ndani ya andiko lake ameonesha ni vipi nchi yetu imewekeza Zaidi kwenye elimu rasmi na kusahau kwenye elimu isiyo rasmi. Pia mwishoni akajiuliza maswali mengi ikiwemo swali hili “ je hakuna kabisa umuhimu wa hii elimu isiyo rasmi katika jamii”

Ingawa serikali katika sera zake na Dira yake ni kuhakikisha kunakuwa na utoaji wa elimu bora kwa Taifa zima, bado kumekuwa na changamoto kadhaa ambazo zinafanya isifikie malengo na hivyo kwa asilimia Fulani elimu isiyo rasmi inakamilisha malengo ya serikali kutokana na huduma zao wanazozitoa. Ni wazi na ukweli kuwa walimu wengi waliopo kwenye mifumo ya elimu iliyo rasmi hawana ari katika ufundishaji wa wanafunzi, hali hii husababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo maslahi binafsi na mazingira magumu ya kazi ambapo sehemu zingine huduma za kijamii hazipatikani kwa urahisi hali hizi hupelekea uhaba wa walimu katika baadhi ya maeneo na wanafunzi hukosa kile walichosatahili. Lakini pia sababu za kimazingira na kiuchumi.

FAIDA KWA JAMII NA SERIKALI ENDAPO SERA ITABORESHWA KWA VITUO VISIVYO RASMI
  • Kwa jamii, huwa ni chanzo cha ajira kwa Watanzania wengi ambao wamesomea ualimu na wapo mtaani bila kuwa na ajira rasmi.
  • Huwapa fursa wale wanaotaka kujiendeleza kielimu kwa kupata elimu kulingana na muda wao na uchumi wao,
  • Hufungamana na sera ya elimu na Dira ya Taifa ya maendeleo 2025 kwa kuzalisha wasomi wengi na wataalamu kwa ngazi tofautitofauti.
  • Upatikanaji wa mafunzo katika elimu isiyo rasmi huwa wa gharama nafuu.
  • Lakini pia husaidia kupunguza makundi ya uharifu mtaani.
  • Humsaidia mwanafunzi kupata masomo ya ziada na kufikia malengo yake kimasomo
picha: halisi nikiwa darasa la masomo ya ziada kituoni kwangu.
Kwa upande wa serikali, serikali itapata faida nyingi sana, baadhi ni;
  • Itakusanya kodi kwenye vituo hivyo na kuwa chanzo cha mapato ya serikali
  • Taifa kuwa na watu wengi wenye elimu na kuelimika ili kufikia malengo ya serikali katika Dira yake na sera yake katika elimu na mafunzo,
  • itapanua mianya ya ajira kwa Watanzania wengi hivyo kuondokana na lawama na kero kutoka kwa vijana ambao kwa sasa ni wahanga wakubwa kwa kukosa ajira na tupo mtaani tu,
  • Itawasaidia walimu au wanafunzi ambao walisomeshwa kwa msaada wa mikopo ya serikali kuweza kurejesha mikopo yao kwa urahisi.
MAPENDEKEZO;
  • Kuwepo na sheria za kielimu zitakazoendana na uhitaji na uboreshwaji wa utoaji wa elimu katika mifumo isiyo rasmi
  • Kuwepo na mazingira wezeshi kwa wamiliki wa vituo vinavyotoa elimu katika mfumo usio rasmi kama vile mikopo toka serikalini na ruzuku.
  • Serikali inapaswa kupanua na kuongeza ushiriki chanya kwa wamiliki na wadau wa vituo vinavyotoa elimu katika mfumo usio rasmi
  • Kuwepo na utambuzi wa wanafunzi wenye vipaji na vipawa walio nje na mfumo rasmi.
  • Kuwepo na uwezeshwaji wa kimasomo kwa wanafunzi wanaoenda elimu ya juu ambao wamepitia kwenye vituo vinavyotoa elimu katika mifumo isiyo rasmi
  • Bajeti ya serikali iwe inazingatia namna ya kuwamotisha na kuwaongezea nguvu wamiliki wa vituo vy elimu isiyo rasmi ili waweze kuviboresha, kuviendesha na kutengeneza ajira kwa wengine.
  • Serikali ivitambue na kuvisajili vituo vyote vinavyotoa elimu ya ziada ili kuvifanya vitoe elimu bora kwa wanaojifunza humo.
HITIMISHO
Suala la maendeleo katika jamii yoyote ile ni lazima lizingatie jitihada na fursa zilizopo na rasilimali zilipo. Ikiwa kuna wahisani katika nyanya yoyote ile ambao wana nia njema katika nchi, serikali haina budi kuwatambua na kuwaunga mkono. Serikali iongeze nguvu katika sera zake ili kuweza kuvifikia vituo vinavyotoa elimu katika mfumo usio rasmi (tuition centres) na kuwajengea uwezo na mifumo stahiki waendeshaji wa vituo hivyo.
Picha: halisi nikiwa nafundisha masomo ya ziada(tuition center).

IMG_20220818_114902_827.jpg
 
Upvote 52
Ni kweli kabisa. Serikali iangalie namna nzuri ya kuboresha vituo hivyo,kwani wengi wetu tumepitia huko
 
Kuna jamaa wengi tu tena wapo ofisi za serikali viongozi niliwahi kusoma nao pale mchikichini. Mazingira ya uwezeshwaji yakiwepo,serikali itanufaika sana, na kuwa na wasomi wengi. Maana wengine waliacha shule Kwa changamoto mbalimbali,wanaweza kutumia vituo hivi kujiendeleza
 
Back
Top Bottom