UTANGULIZI
Masiku yamepita huku nikitamani sana kuandika chochote kuhusu Uyahudi na Wayahudi. Kuandika kuhusu chimbuko lao, kuandika kuhusu uhusiano wao na wana wa Israeli,kuandika kuhusu itikadi zao, kuandika kuhusu madai yao kwa nabii wa Mola muumba Musa mwana wa Imraan mwana wa Quhaata mwana wa Lawi mwana wa Yaqoub mwana wa Is'haak mwana wa Ibrahiim.
Lakini kalamu zimeshanyanyuka na wino umeshakauka na historia iliandikwa kitambo sana na wakubwa zetu kwa ubora, wakubwa zetu kwa maarifa na wakubwa zetu kwa umri, na nachokifanya mimi ni kurejea kwao na wala sitaandika jipya ambalo wao hawakuliandika,yaani kwa ufupi sitazua.
Maneno nitakayo yahudhurisha kwenu katika mfululizo wa anuani hii "KUYAFUNUA YALIYO FUNIKWA" ni natija au zao la utafiti wangu wa muda mrefu juu ya historia ya watu hawa. Lakini marejeo yangu hasa hasa yamemili katika vitabu viwili, ambavyo nitavitaja mwishoni mwa mada hii, yaani nikiwa nahitimisha somo hili.
Nini maana ya Uyahudi?
Katika kudurusu tamko hili la "Uyahudi" nitapita katika mapito mawili tofauti, pito la kilugha na pito la kiistilahi.
Maana ya Uyahudi kilugha
Wametofautiana wanazuoni juu ya tamko hili, wapo wanaosema tamko hili limetokana na lugha ya kiarabu katika tamko "al Huud" lenye maana ya toba (kutubia) na kurejea katika utiifu (kutokana na maovu aliyo yafanya mtu).
Wengine wakakataa na kusema hakika tamko hili si lenye asili ya Kiarabu, bali limetokana na mmoja wa watu kutoka katika ukoo (uzao) wa wana wa Israeli naye si mwingine bali ni "YAHUUDHA" (Huyu tutamuelezea kwa undani huko mbeleni) au tamko "Uyahuud/Yahuud" limetokana na ile dola iliyo anzishwa kusini mwa nchi ya Palestina baada kupita nabii Suleyman na hii ndiyo kauli yenye nguvu.
Maana ya Uyahudi kiistilahi
Uyahudi kiistilahi maana yake ni wale watu wanao dai ya kuwa wana mfata nabii Musa.
Sehemu ya pili post #28
Sehemu ya tatu post #113